ZIKIWA zimebaki siku 24 tu, kabla ya kufunguliwa kwa msimu wa Ligi Kuu Bara 2022/23 kupitia mchezo wa Ngao ya Jamii utakaozikutanisha Simba na Yanga Agosti 13, mwaka huu, uongozi wa Yanga umeibuka na kuchimba mkwara mzito kuwa wao wako tayari kwa mchezo huo hata leo, huku wakitamba kuendeleza maumivu.

Yanga na Simba wanatarajiwa kukutana katika mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, ambapo Yanga wanatarjia kuwa wenyeji.

Kikosi cha Yanga kinatarajia kuanza rasmi kambi yao ya kabla ya msimu leo Alhamisi kwenye kijiji cha Avic Town, huku Simba wao leo Alhamisi wakiwa wanakamilisha wiki ya kwanza tangu waanze kambi yao jijini Ismailia nchini Misri.

Ofisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa baadhi ya watu kuhusiana na wao kujinadi suala la kuanza kambi mapema na kuwaaminisha watu kwamba sisi hatutimizi majukumu yetu ipasavyo.

“Lakini nikuhakikishie kuwa tumejipanga vizuri sana na faida nyingine kubwa ambayo tunayo ni ukweli kwamba kikosi chetu wala hakihitaji mambo mengi, yaani hivi tulivyo wachezaji wetu wanaweza kutoka wanakotoka tukajikusanya tukacheza mechi na kuwapa maumivu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa