Klabu ya soka ya Yanga imepanga kumpongeza kocha wa klabu hiyo Nasserdine Nabi leo kwenye mchezo dhidi ya KMC, Katika mchezo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa leo mida ya saa moja kamili.yangaKlabu hiyo imepanga kumpa heshima kocha wa timu hiyo ambaye amefanikiwa kuiongoza timu hiyo kucheza michezo 43 ya ligi kuu bila kupoteza, Hivo leo katika mchezo dhidi ya KMC klabu hiyo kupitia afisa habari wake Ali Kamwe wamepanga ikifika dakika ya 43 ya mchezo mashabiki wasimame na kupiga makofi kumpongeza kocha huyo.

 

Hii imekuja siku chache baada ya uvumi kua mkubwa kua kocha huyo raia wa Tunisia anakaribia kufukuzwa na klabu ya Yanga. Huku sababu ikiwa ni kocha huyo kutofanya vizuri katika michuano ya kimataifa.yanga, Yanga Kumpongeza Nabi Leo Dhidi ya KMC., MeridianbetLakini baadae klabu hiyo ilikanusha taarifa hizo na kusema itaendelea na kocha huyo, Na leo watampa heshima Nabi kwa kuheshimu kile alichowafanyia Yanga kwa kuwaongoza wananchi kutopoteza michezo 43 ya ligi kuu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa