Yanga Kweli Wanautaka Ubingwa Tena

Mabingwa watetezi, Yanga SC wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC usiku wa jana kwenue Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Nyota wa kimataifa wa Uganda, Allan Okello ‘Star Boy’ aliibuka shujaa kwa mara nyingine tena akifunga mabao mawili dakika ya 53 na 84 na kuwa mchezaji bora wa mchezo huo kwa mara nyingine tena.

Yanga Kweli Wanautaka Ubingwa Tena

Bao lingine lilifungwa na kiungo wa Kimataifa wa Kenya, Duke Abuya dakika ya 26, huku bao la Namungo FC likifungwa na Hassan Salum Kabunda dakika ya 39.

Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 60 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ikiwazidi pointi mbili watani wao, Simbna SC baada ya timu zote kucheza mechi 25 sasa.

Msemaji wa Yanga Ali Kamwe aliutaja ubingwa huo kama sehemu ya kuendelea kupambania malengo yao ambayo wamejiwekea msimu huu ya kuchukua ubingwa kwa mara nyingine na itakuwa mara ya tano mfululizo kama watafakikiwa kufanya hivyo.

Yanga Kweli Wanautaka Ubingwa Tena

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa upande wao Namungo FC baada ya kupoteza mchezo wa jana wanabaki na pointi zao 25 baada ya kucheza mechi 25 kadhalika wakiwa katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini ‘Play Off’ na mshindi wa jumla atasalia ligi kuu.

Yanga Kweli Wanautaka Ubingwa Tena

Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.