Yanga SC inajiandaa kwa pambano la ligi kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar litakalochezwa kesho, huku kocha wake mkuu, Pedro Soares, akisisitiza lengo la timu ni kuhakikisha wanapata alama tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha Pedro amesema: “Siku zote lengo letu ni alama tatu na kesho haitakuwa tofauti lakini ni muhimu kwetu kuwa kileleni bila kujali matokeo ya kesho. Tumemaliza raundi ya kwanza ya ligi tukiwa kileleni mwa msimamo japo halitupi ubingwa lakini linatupa imani kubwa.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar, Awadhi Juma, alisema morali ya kikosi chake ipo juu kwa asilimia mia moja, akionyesha kuwa wamejiandaa kikamilifu kwa pambano hilo lenye ushindani mkubwa.
Aidha, mchezaji wa Mtibwa Sugar, Haruni Lyawatwa, amesema timu yao imejiandaa vizuri na hawana wasiwasi, licha ya uzofu uliopo, jambo linaloongeza matumaini kwa mashabiki wake.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na msimamo wa timu hizo katika msimu huu, huku kila upande ukilenga alama tatu muhimu. Yanga akiwa na fasi ya kwanza na point 37 huku mtibwa akishikilia nafasi ya tisa akiwa na point 21.

