Yanga Yaibua Sababu za Changamoto Licha ya Mwendo Bora Ligi Kuu

Uongozi wa Yanga umeweka wazi sababu mbalimbali zilizoathiri mwenendo wa timu hiyo licha ya kufanya vizuri katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26.

Yanga Yaibua Sababu za Changamoto Licha ya Mwendo Bora Ligi KuuKupitia taarifa rasmi iliyotolewa Machi 23, 2026, jijini Dar es Salaam, uongozi huo umeeleza kuwa timu imefanikiwa kucheza michezo 16 bila kupoteza hata mmoja, ikishinda mechi 11 na kutoka sare tano, huku pia ikiwa kinara wa kufunga mabao mengi (32) na kuruhusu mabao matatu pekee.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo, Yanga imekiri kukumbana na changamoto kadhaa, ikiwemo ratiba ngumu ya mechi. Ndani ya siku 21 pekee, timu ilicheza michezo saba mfululizo, ikihusisha mechi za Ligi Kuu pamoja na Kombe la Shirikisho la CRDB, sambamba na safari ndefu za zaidi ya kilomita 4,462 kwa ajili ya mechi za ugenini.

Yanga Yaibua Sababu za Changamoto Licha ya Mwendo Bora Ligi KuuAidha, tatizo la majeraha limeendelea kuiandama timu hiyo, ambapo jumla ya wachezaji wanane muhimu wamekuwa nje ya uwanja kwa nyakati tofauti, huku watatu wao wakitarajiwa kukosa michezo iliyosalia hadi mwisho wa msimu.

Yanga Yaibua Sababu za Changamoto Licha ya Mwendo Bora Ligi KuuMbali na hilo, uongozi umebainisha uwepo wa changamoto za kiufundi zilizochangia timu kushindwa kucheza kwa kiwango kilekile katika baadhi ya michezo, hali iliyosababisha kupungua kwa ubora wa uchezaji licha ya kupata matokeo chanya.

Kutokana na hali hiyo, Yanga imechukua hatua ya kuimarisha benchi la ufundi kwa kumuingiza Kocha Abdihamid Moalin kama kocha msaidizi ili kuongeza nguvu na ubunifu katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu Pedro Goncalves.

Yanga Yaibua Sababu za Changamoto Licha ya Mwendo Bora Ligi KuuMwisho, klabu hiyo imewahakikishia mashabiki na wanachama wake kuwa itarejea kwa nguvu zaidi katika mzunguko wa pili wa ligi, ikiwa na dhamira ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kufanya vizuri katika mashindano ya ndani.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.