Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga umetangaza kifo cha mwanachama wake, Haji Omari Ramadhani Mpili, aliyefariki dunia usiku wa Jumapili, Septemba 27, 2026, katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo, mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika leo, Jumatatu, Septemba 28, 2026, majira ya saa 10:00 jioni, katika Makaburi ya Msikiti Mkuu yaliyopo Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.
Katika taarifa hiyo, uongozi wa Yanga umeeleza: “Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa mpira kwa msiba huu mzito wa kumpoteza mwanachama wetu.”
Uongozi wa klabu hiyo pia umeziomba familia pamoja na wote walioguswa na msiba huo kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, huku ukitoa pole kwa familia ya marehemu kwa kumpoteza mpendwa wao.
“Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Haji Omari Ramadhani Mpili mahala pema peponi. Amina,” imeeleza sehemu ya taarifa ya uongozi wa Yanga.


