Hakuwa na maisha hakuwa na chochote wakati anaondoka Paris kuja kujiunga na Leicester City ya nchini Uingereza, mfukoni alikuwa huenda na buku tano tu ya kupata lunch na maji, hakuwa na chochote tena Mwanaume huyu kutoka Ufaransa.

Mini

Kwa mara ya kwanza raia mmoja ambaye ni Shabiki wa Leicester alikutana na Kante kwenye usafiri wa umma kuelekea uwanjani kwa ajili ya mechi au mazoezi, Shabiki yule akaona isiwe tabu, akaingia showroom na kumpa Kante zawadi ya gari.

Mini, N’Golo Kanté na Mini Cooper ya Shabiki Yule, Meridianbet

Shabiki yule hakuwa na kipato kikubwa sana ila Mini Cooper ingemsaidia Kante kuepuka adha za usafiri wa umma, kuepusha adha za kuchelewa mazoezini, Kante alimshukuru mno Shabiki yule, asiyejua anaitwa nani wala anatokea wapi, ni wema tu

Wema hulipwa kwa wema, baada ya Leicester City kutwaa ubingwa wa England, Boss wao aliwapa zawadi za BMW kila Mchezaji ila Kante aligoma yeye akasema hii Mini Cooper yangu ina thamani sana kwakuwa kuna mtu alivuja jasho lake, ni heshma nikiendelea kutumia hii.

N'Golo Kanté na Mini Cooper ya Shabiki Yule

Nikwambie tu Ngolo Kante ni Mshindi wa Kombe la Dunia, mshindi wa EPL mbili, mshindi wa EUROPA lakini hajaibadili gari yake hiyo tangu 2015 alivyopewa na Shabiki asiemjua kabisa, gari ina miaka sita na bado yupo nayo, akiamini analipa fadhila kwa Shabiki yule.

N'Golo Kanté na Mini Cooper ya Shabiki Yule

Maisha yake ya London akiwa na Chelsea kuna siku moja alipokea DM ya Shabiki mmoja aliemuomba Kante aende nyumbani kwao kupata dinner, Ngolo hakuona tabu alimjibu Bwana Derrick Mackley anaepatikana mitaa ya Fulham road karibu tu na Stamford Bridge

Familia yake haikuamini kumwona Kante anabisha hodi mlangoni, kwenye begi akiwa amebeba jezi za Chelsea kama zawadi yao, kisha akala na baadae alicheza PlayStation na familia ile, walihisi wapo kwenye ndoto, walihisi sio Kante ila baadae alimaliza kucheza na akaaga kisha akaondoka zake.

Mini

Huyo ndiye Ngolo Kante, licha ya ubora mkubwa kwenye kikosi cha Ufaransa 2018 wanabeba kombe la dunia yeye alichagua kukaa kimya, aliona aibu hadi kupiga picha na Kombe la Dunia, mpaka wenzie wakalichukua na kumpa apige nalo picha, Binadamu huyu bwana.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Mini, N’Golo Kanté na Mini Cooper ya Shabiki Yule, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa