Inter Milan wanatarajia kuwa na mashabiki 1000 pale San Siro kusherekea ubingwa wao wa Italia kwenye mechi dhidi ya Udinese, Je, hii itakuwa mechi ya mwisho ya Conte?

kwa mujibu wa chapisho la La Gazzetta dello Sport, Conte anataka kusalia pale Giuseppe Meazza na kuendelea kuchapa kazi na Inter.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, pande zote mbili, kocha pamoja na raisi Steven Zhang wanashawishika kuendelea na mradi uliopo mbele yao baada ya mafanikio ya msimu huu.

Nini Hatma ya Conte Inter Milan?

Wakati kocha huyu anayetokea Lecce akifikiria mipango yake juu ya ushindi mkubwa zaidi msimu ujao, baada ya kupata hamasha na ushindi wa sasa, kuna mashaka kidogo kuhusu hatama yake klabuni hapo.

Hata hivyo, ripoti zinataja kuwa Conte anaweza kushawishika zaidi ikiwa atahakikishiwa hatma ya wachezaji kadhaa, wa msingi wakiwa ni Romelu Lukaku, Nicolo Barella na Lautaro Martinez ili kubaki hapo.

Conte anahitaji ahadi ya Zhang hasa katika suala zima la uchumi wa klabu na namna msimu ujao utakavyofadhiliwa, baada ya hapo atakuwa kwenye nafasi ya kutambua ikiwa anasonga mbele na Inter au la.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Conte, Nini Hatma ya Conte Inter Milan?, MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa