Mabadiliko ya mpira wa kisasa yameleta ukatili kwenye dunia ya soka. Siku hizi kitu kimoja pekee hakikutoshi kuwa mchezaji. Siku hizi uimara wa mchezaji hautambuliki tena kwa kufanya majukumu yake ya msingi.

Unashangaa? Ndiyo uimara wa mchezaji hautambuliki kwa kufanya majukumu ya msingi. Utaniambia vipi uimara wa mchezaji unatambulika kwa kufanya majukumu ya msingi kama beki bora siyo yule anayekaba tena bali anayecheza mpira?

Ninja

Utaniambia vipi uimara wa mchezaji unatambulika kwa kufanya majukumu ya msingi kama mshambuliaji bora si yule anayefunga tu bali ni yule anayekaba?? Hadi magolkipa bora siku hizi, si wale wanaodaka tena bali ni wale wanaocheza mpira. Mpira wa kisasa huu?

Kwasababu hiyo, kazi ya akina Wan Bissaka haithaminiki pale United. Kwasababu hiyo, Ujerumani walithubutu kumuacha Leroy Sane waliposafiri kwenda World Cup.

Ni mpira wa kisasa huu uliomfanya Pep Guardiola na Wahispaniola wamchezeshe Andres Iniesta namba tisa. Andres Iniesta namba tisa kikosini akiwepo David Villa kweli?

Ninja

Kwasababu hii, Abdallah Shaibu Ninja haonekani beki anayecheza mpira wa zama zake. Soka la leo linadai Abdallah Shaibu ni beki wa kizamani, yeye na Adeyum Saleh.

Naliheshimu sana soka la kisasa na mimi ni muumini mkubwa sana wa mpira wa kisasa. Lakini kila ninapomtazama Abdallah Shaibu Ninja, naishia kumtazama kwa jicho la huruma sana.

Ninja anakaba ardhini, anakaba hewani. Anaijua vita ya nguvu na anaijua ‘sanaa nyeusi’ ya ukabaji anayoihusudu sana kocha Sean Dyche. Kwangu mimi, Ninja ni beki wa kati aliyekamilika.

Bahati mbaya zaidi kwake, anacheza eneo ambalo haliitaji mabadiliko sana kwenye timu. Ni eneo ambalo linahitaji wachezaji kuzoeana kuliko kawaida, hivo ni mara chache sana mgeni atapata nafasi.

Ninja

Bahati mbaya nyingine zaidi kwake, Eneo analocheza ndilo eneo lenye wachezaji wawili imara zaidi Young Africans. Katika umri wake wa miaka 22, ni umri ambao alitakiwa awepo uwanjani. Hapaswi kuwa anasubiri tena.

Ninja anatambua hilo ndio maana kila anapopewa nafasi haichezei. Anajitoa sana, anajituma sana, anamfikirisha kocha sana. Hiki ndicho unatakiwa ufanye ukipewa nafasi.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa