Beki kisiki wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ hakuwa sehemu ya msafara wa juzi Jumanne wakati Yanga ilipoondoka.

Tunafahamu kuwa beki huyo mara baada ya kumaliza mchezo na Azam alipowasha simu tu akakutana na ujumbe wa msiba wa dada yake.

yanga

Beki huyo alisafiri kurudi kwao Zanzibar kuhudhuria mazishi na hapohapo Yanga ikafanya mpango B kwamba wakati wowote beki huyo akirejea asafirishwa ili kuwawahi wenzake Mbeya.

“Baada ya kurejea Dar, Tumetumia kila njia kumsafirisha ili kuwahi wenzake pale Mbeya, ilikuwa ni lazima asafiri, hili halina kipingamizi,” alisema Ofisa mmoja wa juu wa Yanga.

yanga

Ninja ameungana na wenzake jana na Yanga imeweka kituo Mbeya ambapo hapo wanajifua kabla ya kuwafuata Prisons.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa