Mchezaji namba 1 kwa ubora duniani (mchezo wa tenesi kwa wanaume), Novak Djokovic, hatotetea ubingwa wake wa Madrid Open baada ya kujitoa kwenye mashindano ya mwaka huu.

Djokovic ameomba radhi kwa kushindwa kusafiri kwenye nchini Hispania kwenye mashindano hayo ambayo yataanza Jumapili hii, wiki 4 kabla ya mashindano ya French Open 2021 kuanza kutimua vumbi.

“Ni miaka miwili sasa, muda umekwenda sana. Naimani tutaona mwakani” alisema Djokovic. Mwaka jana, mashindano ya Madrid Open hayakufanyika kutokana na hali ya maambukizi ya COVID19 nchini humo.

Novak Djokovic, Novak Djokovic Kuikosa Madrid Open 2021., Meridianbet
Djokovic akiwa na taji lake la Madrid Open 2019 baada ya kumfunga Stephano Tsitsipas kwenye mchezo wa fainali.

Wikiendi iliyopita, Novak Djokovic aliondolewa kwenye hatua ya nusu fainali kunako mashindano ya Serbia Open baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Aslan Karatsev. Huu ni mfululizo wa vipigo baada ya kutolewa kwenye mashindano ya Monte Carlo kwa kufungwa na Dan Evans.

Mwezi Februari, Djokovic alibeba taji la 18 baada ya kuibuka kidedea kwenye mashindano ya Australian Open. Kama sehemu ya kujiandaa na mashindano ya French Open (Mei 30), Djokovic anategemea kucheza Rome na Belgrade mwezi ujao.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa