Fowadi wa Kaizer Chiefs Samir Nurkovic amesema wanapaswa kukaa umakini na wasifikirie sana juu ya historia wanapojiandaa kuchuana na Simba SC katika mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Caf Jumamosi.
Nurkovic Hana Habari na Rekodi ya Simba ya Comeback
Nurkovic dhidi ya Onyango

Amakhosi walipata ushindi mnono wa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza nchini Afrika Kusini, na mashabiki na wataalamu wengi wanaamini mchezo wa pili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa sio chochote isipokuwa tu kukamilisha utaratibu.

Wekundu wa Msimbazi, hata hivyo, wana matumaini ya kuandika tena historia kwa kupindua matokeo tena, sawa na 1979 walipofungwa 4-0 na Mufulira Wanderers nyumbani lakini walishinda mchezo wa pili 5-0 kusonga mbele.

Comeback ya Simba ilifanyika mbele ya Rais wa Zambia wakati huo Kenneth Kaunda. Mabao ya wababe hao wa Mtaa wa Msimbazi yalitiwa kimiani na Thuwein Ally, aliyefunga hat-trick, na George ‘Best’ Kulagwa, aliyefunga bao moja.

Nurkovic Hana Habari na Rekodi ya Simba ya Comeback

Lakini, mshambuliaji wa Waserbia wa Amakhosi anasisitiza lazima wazingatie na kuhakikisha wanaendelea kutoka hapo walipoishia kwenye mkondo wa kwanza.

“Tunatarajia mchezo wa marudiano na tumefanya bidii kujiandaa na mechi hii,” Nurkovic alisema kabla ya mechi.

“Tutafanya kila kitu kufikia hatua ya nusu fainali. Tunataka kuendelea kutoka pale tulipoishia kwenye mechi iliyopita. Hatuwezi kufikiria juu ya mambo hayo sana. Tunachopaswa kufanya ni kukaa umakini.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa