Callum Hudson-Odoi hatachukuliwa hatua yoyote kuhusu shtuma zake dhidi ya ubakaji, winga wa Chelsea amethibitisha.

Hudson-Odoi, 19, alikamatwa Mei 17 na kuruhusiwa kwa dhamana.

Mchezaji huyo wakimataifa wa Uingereza ameandika katika ukurasa wake wa Twitter na kusema: “Wakati vitu vikubwa vikitokea Duniani kwasasa, unafahama shutma kubwa zilizkuwa dhidi yangu.

“Nilikuwa kimya nikisaidiwa na polisi katika kipindi chote cha upelelezi, nikijua kuwa kuna siku itafika jina langu halitakuwa na hatia.

“Kufuatia upelelezi uliojitosheleza, polisi wamesema hawatachukua hatua yoyote dhidi yangu.”

, Odoi yuko Huru, Meridianbet

Katika taarifa ya Metropolitan Polisi imesema: “Mtu aliyekamatwa Jumapili ya Mei 17 kwa shutma za ubakaji amechiwa huru bila kuchukuliwa hatua.

“Tukio hilo halitachunguzwa tena na polisi.”

Hudson-Odoi, ambaye amecheza Uingereza mechi tatu na Septemba alisaini kandarasi ya miaka mitano na Chelsea, alikuwa mchezaji wakwanza kwa Premier League kugundulika kuwa na Virusi vya Corona.

Odoi aliongeza kusema: “Napenda kutumia jukwa hili kuwashukuru wote waliosimama na mimi kipindi kigumu na kunisaidia.”

46 MAONI

  1. Duuh pole sana ndiomaana watu wengi wanasema sio kila anaeenda jela hana hatia wengine wamesingiziwa pole sana ##meridianbettz

  2. Me sijaelewa kama mtu anakamatwa si lazima kisibitisho kiwepo mbele yake sa kwanini haende jela mwisho wa siku haonekane hana atiya..!odoi unàmungu sana endelea kusali ktk imani yako

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa