Mikataba ya Matangazo

Michezo ni miongoni mwa biashara kubwa na nzito sana ambayo wenye uelewa na akili juu ya biashara hiyo na aina ya uwekezaji unaofanywa hapo anaweza kuona kama mambo yanayofanyika ni ya kimaono tu. Wengi duniani wameweza kufanikiwa sana kutokana na michezo wanayoicheza.

Baadhi ya michezo ambayo kiukweli inalipa sana duniani ni pamoja na soka, mpira wa kikapu, tenisi na gofu. Hiyo ni baadhi ya michezo ambayo kwa kiasi kikubwa huangaliwa sana na kufuatiliwa na mashabiki lakini pia huweza kuvutia wawekezaji na wadhamini kujitokeza ili kuangalia kama wanachokifanya kinaweza kuwa na tija kwenye biashara yao katika ngazi zote yaani mtu mmoja mmoja au hata katika kundi pia. Baadhi ya wanaonufaika na pesa za matangazo ya biashara:

Roger Federer

Mkongwe huyo wa tenisi amekuwa akila pesa zake nyingi kutokana na mikataba mingi ya kibiashara ambayo huhusisha kutangaza bidhaa zao ili ziweze kupata nafasi ya kuwika katika mataifa mengine. Kutokana na anachokifanya kwa sasa anaendelea kushikilia nafasi ya juu ambayo inamfanya apate $65M ambazo ni hela nyingi kabisa ndani ya uwekezaji wake huo. Kwa mengi aliyoyafanya itakuwa vigumu aliyoyafanya kusahaulika kwa urahisi.

LeBron James

Mbali na mikataba hiyo bado yeye mwenyewe ana mambo yake ya pembeni ambayo yanamuingizia kipato kikubwa. Jambo ambalo amelifanya na lina upekee ni kujenga shule ambayo anawasaidia watoto wa wasiojiweza na wenyeji wengi wa mitaa ambayo yeye mwenyewe kwa asili yake ametokea huko. Kwa kutambua uhitaji huo akaamua kufanya analoweza kutimiza ndoto zao. Kupitia matangazo ikiwemo na Nike anatengeneza kiwango cha $52M peke yake.

Cristiano Ronaldo

Yeye ni miongoni mwa wanasoka wengi ambao wamefanikiwa sana upande huo wa matangazo na uhusiano wa kimapato wanaoupokea kutoka Nike na CR7 Underwear. Kupitia jambo hilo anakuwa juu kabisa kati ya watu walio upande wa soka. Kati ya wanasoka wengi waliopo basi yeye ameweza kukaa katika nafasi ya juu. Anaingiza kiasi cha $47M kutokana na hilo, na ni tofauti na mishahara yake ya kila siku.

Tiger Woods

Gofu inaheshimika kutokana na uwepo wa watu kama hawa ambao wameipa heshima kwa kufanya kile ambacho kinastahili kufanywa. Ameweza kushinda vikombe vingi sana na kupata mafanikio sana kutokana na uwezo wake. Anakaa katika historia ya watu wanaokula hela kubwa ya matangazo ambayo ni $42M.

3 Komentara

    Michezo inatengeneza afya kuwa poa.

    Jibu

    Pesa zinapatikana kwenye

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe