Baada ya Ozil kukamilisha uhamisho wake kwenda kwa Mbwana Samatta, Fenerbahce amesema kuwa anaondoka klabuni hapo bila kinyongo licha ya kubaniwa mda wa kucheza kwa karibu mwaka mzima.

Ozil amewaaga timu yake, na kuwaandikia ujumbe wa uchungu, ambao undadhihirisha mapenzi aliyokuwa nayo na klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa takribani miaka saba na nusu.

Safari yake Arsenal anaiona ilikuwa safari ya furaha sana, licha ya ukweli kuwa dakika za mwisho mambo yalibadilika. Mkataba wake ambao ulikuwa na mshahara wa £350,000 kwa wiki ulikuwa unaisha mwisho wa msimu huu.

mesut ozil fenerbahce

Sehemu ya Ujumbe wa Mesut Ozil kwa Arsenal na Mashabiki wake

“Ndugu wana Arsenal
Miaka 7.5. Karibu siku 3000. Inakuwa kitu kigumu kuandika ujumbe huu baada ya mda huo mrefu hapa London. Tangia wakati nilipowasili, imekuwa kama nyumbani. Nilikaribishwa kwa mikono miwili na wafanyakazi wote wa Arsenal, wachezaji wenzangu, na muhimu zaidi ni mashabiki.

Wakati wote nitamshukuru Arsene Wenger kwa imani aliyoiweka juu yangu mwaka 2013. Nimekuwa kama mtu mzima London Kaskazini, mahali ambapo wakati wote nitapaita nyumbani.

Kuwa na Arsenal kwa mda huo mrefu inamaanisha nimepitia mengi sana katika kupanda na kushuka. Kwa zaidi ya mechi 250, magoli 44 na pasi za mwisho 71 baaadaye, ni wakati sasa Arsenal na mini tunaagana.

Kwa pamoja, tuliondoa uhaba wa taji wa miaka 9, na kurejesha taji lililokuwa likisubiriwa sana kwa mashabiki waliostahili.

Ni vigumu sana kwangu kuelezea kwa maneno mapenzi niliyonayo kwa klabu hii na mashabiki. Nitawezaje kuelezea miaka 8 ya furaha kwenye barua moja? Wakati sitakuwa mchezaji tena wa klabu, nitaendelea kutoa sapoti katika kila mechi wanayocheza. Nitaendelea kuwa Arsenal maisha yangu yote.

Wakati huu ni muhimu wote kuwa nyuma ya timu kuliko wakati mwingine wowote. Msimu huu ni mgumu kwa kila timu ya Ligi ya Primia, na ndiyo maana wote tutakuwa tukiwasapoti kikosi kilichopo sasa na wafanyakazi bila kujali matokeo……..”


 

MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

15 MAONI

  1. Kijana wa Wenger hatimaye ameondoka baada ya makocha waliokuja baada ya Wenger kuona hana msaada kwa Timu licha ya kulipwa hela nyingi

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa