Kama ni shabiki ndakindaki wa soka toka miaka ya 2000 basi jina la Park Ji-Sung si geni sana kwako! Wakati dunia ikiendelea kufurahia na kushangaa maajabu yanayoletwa na mkorea Son Heung-Min, bado jina la Park Ji-Sung litaendelea kukumbukwa.

Added: Huyu ni mchezaji wa kimataifa wa Korea Kusini aliyekuwa kama kiungo. Safari ya Park Ji-Sung ilianza huko Korea ambapo alichezea timu ya chuo cha Myongij, aliendelea na jitihada zake huko Japan katika klabu ya Kyoto Purple Sanga. Baada ya hapo milingo mikubwa ilianza kufunguka na akasajiliwa na klabu ya PSV Eindhoven ya nchini Uholanzi. Katika timu hii alifanikiwa kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2004/2005.

Park Ji-Sung
Park Ji-Sung akisherehekea goli

Nusu fainali ikawa chachu ya mafanikio kwa nyota huyu wa kikorea, jicho la kocha wa Manchester United, Sir. Alex Furgeson na Julai ya mwaka 2005 akamsajili kwa dau la Euro Milioni nne. Akiwa Manchester United, Ji-Sung alipata mafanikio mengi sana. Akafanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza wa kikorea kushinda taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 2007/2008, na pia akashinda kombe la vilabu la dunia 2008.

Ji-Sung alikuwa na wakati mzuri sana Manchester United, lakini kuna kitu ambacho watu wengi hawakuweza kujua kuhusiana na mchezaji huyu. Katika moja ya majadiliano aliwahi kusema wakati mgumu kumkuta akiwa Klabuni hapo ilikuwa ni kipindi cha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea ambayo hakuwa kwenye kikosi kilichopangwa kucheza siku hiyo.

Anasema siku hiyo alikuwa na huzuni sana. Hat baada ya kushinda taji hilo hakuwa na furaha wala huzuni. Alichanganyikiwa, hakuweza kujua ni hisia gani awe nazo. Alijua kuwa walishinda ubingwa wa ulaya lakini hakuwepo kwenye kikosi hicho kilichobeba ubingwa.

Baada ya takribani misimu saba akiwa na Manchester United, mwaka 2012 Ji-sung aliondoka Manchester United na kwenda kujiuunga na Queen Park Rangers, baada ya kukosa namba kikosini kwa muda mrefu akiwa huko Old Traford.

Akiwa na timu ya taifa, mchezaji huyu amefanikiwa kufunga goli katika mara zote ambazo Korea ilishiriki kombe la dunia. Alifanya hivyo mwaka 2002 baada ya kufunga Ureno, akarudia tena mwaka 2006 na 2010. Jambo hili linamfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Asia kufunga mfulululizo katika michuano mitatu ya kombe la duniani.

Mpaka sasa Ji-Sung anaendelea kuwa balozi wa Manchester United. Kwa mtazamo wako unahisi Son Heung Min ataweka ufalme wake huko Korea?


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Park Ji-Sung, Park Ji-Sung: Mzee Wa Mechi Kubwa, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa