Mwandishi wa vitabu wa kifaransa Anais Nin vidole vyake viliwahi kuandika maandishi yanayosema, “Maisha huchanua na kusinyaa kutokana na ujasiri wa mtu husika”.

Maandishi haya siku kama leo mwaka 1981 yalitimia mbele ya uso wa Bi Juliete Evra kwasababu ilibidi awe jasiri kuhakikisha dunia ya soka inachanua kwa kutupa zawadi ya mtoto Patrice Evra pale kwenye kipande kidogo cha ardhi ya mji Dakar, Senegal.

evra, Patrice Evra, Alivyobadili Fikra, Meridianbet
Evra akiwa Monaco

Maandishi hayo ya Anais Nin yanaweza kupewa nguvu na moyo wa marehemu Steve Jobs ambaye daima aliamini kila mtu alizaliwa ili kuweka chapa yake juu ya ulimwengu. Hivyo Patrice Evra hakuzaliwa tu isipokuwa pumzi yake ilishushwa kwenye tumbo la mama yake ili kutimiza maandiko juu ya kipaji chake kikubwa cha soka, ilishushwa kuja kuweka chapa.

Lakini Shaaban Robert katika shairi lake la maisha aliwahi kuandika kuwa “Maisha hayatakwisha bali waishio,” hivyo kumbukumbu zake Evra alizoziweka katika mchezo wa soka zitaishi milele licha yeye na wapendwa wake kutafuna na udongo siku moja.

evra

Mwanasaikolojia wa kimarekani William James yupo ndani ya ushairi wa Shaaban Robert amelala usingizi wa milele kaburini lakini kauli yake ya mtu atabadili maisha yake kama ataweza kubadili namna ya kufikiri bado inavuta pumzi.

Kauli hiyo ina makazi kwenye nafsi ya Partice Evra kwasababu alifanikiwa kubadili fikra zake kwa kitendo cha kutoka Monaco kwenda Man United mwaka 2006 na mabadiliko hayo ya kifikra yalimfnya kubeba vikombe 22 katika maisha ya soka akiwa na vilabu kama Juventus, Man United, Monaco yaliwafanya mashabiki wa West Ham na timu ya taifa ya Ufaransa kumuona tumaini jipya.

evra, Patrice Evra, Alivyobadili Fikra, Meridianbet

Marehemu Nelson Mandela aliwahi kusema: “Michezo inaweza kuwa matumaini,” kwasababu alifanikiwa pia kuwapa matumaini vijana maskini wa kiafrika kuwa wanaweza kufanikwa kupitia mchezo wa soka na michezo mingine.


Unaweza kuwa milionea wakati wowote!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

evra, Patrice Evra, Alivyobadili Fikra, MeridianbetBASHIRI SASA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa