Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anaweza kurejea Juventus mkataba wake ukimalizika pale Old Trafford Juni mwakani. –Kwa mujibu wa wakala wake Mino Raiola.

Pogba ameanza kampeni ya 2021-22 akiwa na fomu nzuri kwa Mashetani Wekundu, akichangia asisti saba katika mechi nne za mashindano yote.

Hatma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 na mabingwa hao wa Uingereza wa mara 20 bado haijulikani, mkataba wake wa sasa ukiwa unatarajiwa kumalizika Juni 2022.

Paul Pogba
Hatma ya Pau Pogba bado haifahamiki United

Wakala Mino Raiola amedokeza kwamba mteja wake anaweza kusaini kandarasi mpya na timu ya Ole Gunnar Solskjaer, lakini wakala huyo maarufu pia amezungumzia uwezekano wa Paul Pogba kurejea Turin.

“Paul Pogba anamaliza mkataba mwezi Juni, kwa hivyo tutazungumza na Man Utd na tutaona nini kitatokea. Juventus? Paul bado anaipenda Turin. Kuna uwezekano kwamba Pogba atarudi Juventus, ndiyo, lakini pia inategemea Juventus wana mpangobgani”

 

Mino Raiola

Pogba hapo awali aliondoka Man United kwenda Juventus mwaka 2012 na alikaa miaka minne na miamba hao wa Italia, akishinda mataji manne ya Serie A na mataji mawili ya Coppa Italia kabla ya kurudi Manchester.

Barcelona, ​​Real Madrid na Paris Saint-Germain pia wanaaminika kufuatilia hali ya mkataba wa Pogba.


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa