Mwandishi mmoja aliwahi kuhoji kuhusu Paul Scholes lakini alichojibiwa hakukiamini. Yule mwandishi alimsogelea tena Socrates ili amsikie vizuri, ni kama masikio yake hayakuamini alichokuwa anasikia.

Paul Scholes, Kiungo Aliyekamilika Idara zote

“si umeniuliza kiungo bora wa katikati kwa sasa duniani? Basi jibu langu halitabadilika, ni mvulana Fulani hivi mwenye nywele nyekundu, anavaa jezi nyekundu pale Manchester, Yule muingereza Paul Scholes. Nadhani anastahili kuichezea timu ya taifa ya Brazil.”

Hakuna aliyetegemea jibu kama lile kutoka kwa mchezaji wa Brazil. Wengi walisubiri amtaje Rivaldo, Ricardo Kaka au Gilberto Silva. Lakini yeye hakumuona kiungo wa Brazil kwenye jedwali moja na Scholes.

Hadithi ya Scholes inaanzia mbali sana katika mashindano ya shule za sekondari Uingereza mwaka 1991. Hapo ndipo mabalaa yake yalionekana na kusajiliwa na academy ya Manchester United mwaka 1991.

Alipiga kazi sana katika timu ya watoto lakini aliachwa ‘kichwa chini akiishangaa ardhi’ Alipowashuhudia washikaji zake wakimuacha na kupandishwa timu ya wakubwa 1992.

Wanae David Beckham, Nicky Butt, Garry Neville,Ryan Gigs na Phil Neville, wote walimuacha akipangiwa ratiba ya kulaa katika timu ya watoto, wao wakapanda kwenda kukipiga ‘theatre of dreams’.

Ilibidi asubiri mwaka mmoja mbele ili apandishwe timu kubwa. Akapandishwa na kukabidhiwa jezi namba 24.

Alilazimika kusubiri nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza iliyokuja baada ya Mark Hughes kujiunga na Chelsea na binadamu mkorofi kuliko wote ‘mfalme mtukutu’ Eric Cantona kupigwa rungu la kukaa nje ya uwanja kwa miezi nane baada ya kumgeuza shabiki begi la mazoezi ya ndondi, akamtupia teke kama wanacheza Kung fu.

Paul Scholes akapata nafasi ya kudumu iliyomuweka Manchester United kwa miaka 20. Pale Manchester amecheza mechi 718, amebeba jumla ya mataji 25 kati ya hayo mawili ya klabu bingwa Ulaya. Ametwaa mataji 11 ya Ligi kuu ya Uingereza, hakuna mchezaji wa Kingereza aliyefikisha idadi hiyo.

Ni Scholes huyu ambaye Zinedine Zidane na ufundi wake wote anakiri kwamba, hakuwahi kukutana na kiungo mgumu kama Paul Scholes. Hata Xavi Hernandez na pasi zake zote anadai kwamba hakuwahi kumuona kiungo aliyekamilika kama Scholes.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Scholes, Paul Scholes, Kiungo Aliyekamilika Idara zote, MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa