Kocha mkuu wa klabu ya Roma, Paulo Fonseca amesema timu hiyo ya Serie A haina mpango wa kumuuza nyota wake Nicolo Zaniolo hali ya kuwa taarifa za uhamisho wa nyota huyo kuzagaa.

Zaniolo amekuwa akicheza katika kiwango kizuri tangu ajiunge na ligi hiyo akitokea kwa mahasimu wa Serie A Inter Milan mwaka 2018, na kujitengenezea ufalme wa kuwa mchezeshaji katika timu ya Giallorossi na Italy

Lakini kiungo mshambuliaji huyo, aliye rudi kutoka kwenye kuuguza majeraha ya goti mwezi huu amekuwa akihusishwa na kutimkia katika ligi ya Premier League na timu ya Jose Mourinho Tottenham imekuwa ikihusishwa na kumsajili kiungo huyo lakini Inter na Juventus pia wanahitaji saini ya mchezaji huyo.

Zaniolo, Paulo Fonseca- Zaniolo Hauzwi., Meridianbet

Fonseca amekataa kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 na roma wanatarajia kumpa dili nyingine mchezaji huyo aliyefunga kwenye mchezo dhidi ya SPAL na Roma kuibuka na ushindi mnono wa 6-1.

“Hatutaki kumuuza Zaniolo au Lorenzo Pellegrini,” Fonseca aliiambia Sky Sports Italia.
“Ni wachezaji muhimu sana kwa malengo ya Roma ya baadaye.”

Zaniolo alitokea benchi baada ya dakika ya 11 ya kipindi cha pili na kufunga goli safi dakika ya 90 kwenye ushindi wa 6-1 katika Serie A wakiwa ugenini kwa mara ya kwanza tangu 1935.

Kulikuwa na mazungumzo ya kuwa Zaniolo hana furaha akiwa Roma pia kumekuwa na tetesi kuwa Zaniolo anamwaruzano na Fonseca.

 


 

Kwa sababu ya thamani ya pesa yako, kwa kila muamala unaofanya wa kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Meridianbet unapata 5% bonasi.

Soma hapa zaidi

55 MAONI

  1. Wameona anaumuhimu katika timu kocha anajua kama katika wachezaji ambao wanafanya vizuri zaidi nae ni miongoni mwao ndio mana hawezi kuunzwa

  2. Lakini kiungo mshambuliaji huyo, aliye rudi kutoka kwenye kuuguza majeraha ya goti mwezi huu amekuwa akihusishwa na kutimkia katika ligi ya Premier League na timu ya Jose Mourinho Tottenham imekuwa ikihusishwa na kumsajili kiungo huyo lakini Inter na Juventus pia wanahitaji saini ya mchezaji huyo.

  3. Kila mchezaj yupo sokon kikubw hapo dau la makubaliano baina ya club na club na kufikiah muafaka pesa ndo kila kitu

  4. Ujue hapa tunaona Kuna makundi mawili upande wa Paulo Fonseca kocha na upande wa wakala wa zaniolo maana hizi tetesi zilikuwa kabla ajapata majeruh stil now linaendelea kusemekana linawezekana likawa kwel ila wanatuficha maana kiungo huyu ntamtambua tokea akiwa club ya inter milan alivyokuwa anafanya maajabu mpk kuingia roma ila ukwel anatambua wakala wake na yeye mwenyew

  5. Kocha kama kocha yupo kwa ajili ya kujenga timu na sio kumzuia mchezaji mahamuzi so Roma bado wanamuitaji sana zaniolo lakini inaonekana kama mchezaji huyo hafurahii kubaki kwenye clabu hiyo

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa