Kocha ambaye kwa sasa maisha yake ya soka yapo katika jiji la Uingereza, akiendelea kupata mafanikio ya aina yake mara baada ya kuwa na kikosi kilichomfanikishia kushinda mataji mengi katika kipindi kifupi sana alichohudumu na klabu hiyo ya soka katika jiji la Uingereza. Kwa sasa amefanikiwa kufika sehemu fulani ya mafanikio yake.

Kocha huyo ana historia ya pekee kwa kufundisha soka lake katika klabu za Barcelona japo hakudumu sana kushuhudia mafanikio zaidi ya kikosi hicho mbalj na kuwa aliwahi kuwa zao la kikosi hicho. Akiwa kama sehemu ya kikosi hicho ameweza kufanya kazi na majina makubwa kama Messi na anatambua kipaji chao ndani ya soka.

Lionel Messi aliweza kuonesha makubwa sana chini ya Pep jambo ambalo lilinfanya kocha huyo atambue kwamba nyota huyo aliweza kuzaliwa na kitu cha pekee ambacho lazima mwisho wa siku kingeweza kuwa chachu ya mafanikio katika timu hiyo. Na hakika jambo hilo lilifanikiwa na limeweza kufikia mahala penyewe.

Guardiola anasema alitambua kwamba kikosi hicho kingeshinda kila kitu tangu mara ya kwanza Messi alipokuwa anacheza na kikosi chao hicho kwa sababu ya uwezo wake ambao aliweza kuuonesha awali. Uwezo wake uliweza kutabiri mafanikio ya mbeleni kwa kadri ambavyo alikuwa akiitumia vema karama yake.

Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or ambaye aliweza kushinda mataji mengi hapo nyuma na ambayo bado anayashinda hadi sasa, aliweza kuanika uwezo katika miaka minne ambayo Guardiola alikuwa kama kocha wa kikosi hicho kwa mafanikio ya namna yake. Kuweza kufikia hatua hiyo kumemfanya bora hadi sasa. Hiyo ni baada ya kocha huyo kumtengeneza nyota huyo kama namba nane wa uongo ambaye haishii kukaa kusubiri kulishwa mipira.

Anasema wakati ameingia kikosini hapo aliambiwa kuna nyota ambaye anafanya vizuri ndani ya kikosi chao lakini bado mdogo. Na akiwa kwenye mizunguko yake alikutana naye kwenye maduka ya Nike na kushangaa sana kwa sababu alikuwa ni kijana mwenye aibu na mdogo sana. Lakini alipokwenda nae Scotland kwa ajili ya maandalizi ya msimu aligundua uwezo halisi wa nyota huyo na kumtabiria makubwa.

Waliweza kuchukua mataji 14 wakiwa na Pep ambayo sehemu ya mataji hayo ni makombe matatu ya ligi na mawili ya klabu bingwa lakini mwaka 2012 aliweza kuondoka klabuni hapo na baadae kujiunga na kikosi cha klabu ya Bayern Munich ambako aliweza pia kutengeneza historia ya pekee.

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa