Ipi hukumu kubwa zaidi kuwahi kutolewa duniani? Hakuna anayejua jibu sahihi. Ila ipo moja tunayoweza kuitumia kama mfano, japo sina hakika kama ndiyo hukumu ya kikatili zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya dunia, ila inafaa kuwa mfano mzuri. Ni ile ya Pontio Pilato kutoka mji wa Judea kwenda kwa Massih Issa Bin Mariam.

Watu walipompeleka nabii Issa mikononi mwake wakitaka auwawe, alisikiliza mashitaka kutoka pande zote mbili. Hakuona kosa linalomkabili nabii Issa kustahili kufa, ila kwa kuhofia kiti chake cha uongozi, alipitisha hukumu ya kifo kama walivotaka wale washitaki. Kumradhi, kama sijasimulia ipasavyo.

Kila nikiifikiria hii habari, kichwani mwangu ananijia muitaliano Perluigi Collina. Yes, referee bora wa mwaka wa FIFA mara sita. Referee bora kuwahi kutokea katika historia ya soka. Referee pekee ambaye hadi anastaafu halaumiwi na timu yoyote kuwa aliwahi kuwaonea.

Subiri kwanza, hapa namzungumzia mtu aliyeongeza dakika 3 katika fainali ya UEFA mwaka 1999 pale Camp Nou, Manchester United wakasawazisha na kupata bao la ushindi mbele ya Bayern Munich. Collina ni mtu asiyetingwishwa.

Labda ujasiri wa maamuzi yake ulitokana na maisha aliyokulia utotoni. Si rahisi kulelewa na mama Mwalimu na baba askari alafu usiwe mtu wa sheria. Asingetetereka maamuzi hata mbele ya akina Duncan Ferguson. Angetenga tuta akiwa anacheka halafu ukimlalamikia anakutwanga kadi akikukaripia. Yule ndiyo Perluigi Collina.

Usidhani alikuwa hivo kwa wachezaji tu, hata waamuzi wenzake walikoma kumtambua. Kabla ya mechi angewaweka wasaidizi wake chini, awape ‘tution’ ya namna timu zote zinavocheza na wachezaji wakuwaangalia kwa jicho la tatu. Ndiyo maana Ronaldo De Lima alijiamini vile mbele ya wajerumani pale Korea Kusini katika fainali ya kombe la dunia 2002.

Marehemu Steve Jobs alisema, “Njia pekee ya kufanikiwa ni kupenda unachofanya”. Nadhani ndiyo maana Collina amefanikiwa. Immagine aliacha kazi ya jeshi na shahada yake ya uchumi ili akawe muamuzi.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma Zaidi

32 MAONI

  1. Namkubali Sana uyo Collina akiwaga kwenye kaz anaga masiala anafanya vile kinavyo fanywa kitekelezwe kipasavyo

  2. Collina Amejizolea umaarufu mkubwa sana hasa kwa style yake ya uamuzi maana alikuwa imara sana na watu walitokea kumpenda kupita maelezo

  3. Collina amechukua umaarufu sana katika kuchezesha kombe la dunia pia ni kocha ambaye yuko makin na wachezaji wajanja ambao wanajiangusha bila sababu namkubal sana 👍 huyu refa

  4. Collina Amejizolea umaarufu mkubwa sana hasa kwa style yake ya uamuzi maana alikuwa imara sana na watu walitokea kumpenda kupita maelezo

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa