Kocha wa Juventus – Andre Pirlo anasema hakuwa na wasiwasi ya kukutana na Barcelona licha ya kutoka sare kwenye Serie A kwa mara ya pili.

Juventus walijikuta wakitafuta matokeo ya sare katika mchezo wa Serie A dhidi ya Hellas Verona wikiendi hii. Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Juve kushindwa kuwafunga Verona kwa misimu miwili mfululizo tangu mwaka 1989.

Pirlo hakufurahishwa na matokeo hayo lakini anasisitiza kutokuwa na wasiwasi atakapo wakaribisha Barcelona wiki hii kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa – UEFA.

“Sinawasiwasi na Barcelona kwa sababu ni michezo miwili tofauti yenye aina mbili tofauti za uchezaji.

“Kama nilivyosema hapo awali, Atalanta na Verona wananamna mbili tofauti za uchezaji ukilinganisha na Barcelona. Kwahiyo unavyocheza na timu ya namna hiyo, unakuwa ni mchezo wa aina yake.

“Unapaswa kujaribu kufanya baadhi ya vitu ambavyo leo tumevifanya uwanjani.”

Kwa sasa, Juve wanashikilia nafasi ya 2 kwa kuzidiwa pointi 3 na AC Millan kwenye msimamo wa Serie A. Akizungumzia matokeo ya Juve kwa mechi za hivi karibuni, Pirlo amesema, ” Sina wasiwasi na matokeo ya sare kwasababu bado tunaitengeneza timu.

“Ni sawa tunaumia kwa kupoteza pointi lakini tupo kwenye njia sahihi tukiwa bado tunatengeneza timu ya muda mrefu.

“Ndio kwanza mchezo wa tano, ninaona mambo mazuri yanakwenda kutokea kwa siku za zijazo.”

Pirlo ataiongoza Juve kwenye mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya UEFA Jumatano hii akiwakaribisha Barcelona jijini Turin. Juve wataikosa huduma ya Cristiano Ronaldo kutokana na taratibu za kujinda na COVID19.


Tsh.160,000,000 Kushindaniwa!

Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.

Kamata Mkwanja wako HAPA🤑

Pirlo, Pirlo Hanawasiwasi Kupambana Na Barcelona, Meridianbet

25 MAONI

  1. Kwa sasa, Juve wanashikilia nafasi ya 2 kwa kuzidiwa pointi 3 na AC Millan kwenye msimamo wa Serie A. Akizungumzia matokeo ya Juve kwa mechi za hivi karibuni, Pirlo amesema, ” Sina wasiwasi na matokeo ya sare kwasababu bado tunaitengeneza timu.

  2. juve kama watazarau hii gemu ya barcelona bac hinaweza watekeo yakawapindukia wao tumeona kwa heallas ulikua si mchezo wa kupata sare kwao makosa mengi yalifanyika mwisho wa siku wakaambulia sare subili tuone kwa barcelona

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa