Ikiwa taarifa zimesambaa kuwa Paul Pogba amegoma kusaini mkataba mpya na Manchester United huku akihusishwa na PSG, kuna kitu kinaendelea katika hili.

Katika hali ya kawaida, tunashauriwa kuwa na akiba ya maneno. Mwaka 2018 kupitia gazeti la Marca, Pogba alinukuliwa akiiambia Canal + ” Ninauhakika sitokuja kucheza soka ngazi ya klabu pale Parc des Princes. Sivutiwi na hilo kwa sababu, baba na mama yangu ni mashabiki wa Marseille kwahiyo Paris haipo kabisa kwenye mipango yangu”

Miaka 3 mbele, 2021 hii hapa na Paul anahusishwa tena na PSG. Mwandishi Dale O’Donnell kupitia ukurasa wa Stretty News, ameripoti kuwa, baadhi ya mashabiki wa PSG wameweka bango kwenye uwanja wa timu hiyo wakishinikiza timu hiyo isijaribu kumsajili mchezaji huyo kwa sababu hawamtaki.

Pogba

Champisho la mashabiki hao linasomeka (kwa Kiswahili) Pogba unapaswa kumsikiliza mama yako, hakutaki hapa. Na sisi pia (hatukutaki)!”

Bado haijajulikana wazi sababu zilizochochea hisia hizi za mashabiki wa PSG kwenye sakata hili lakini pia 2019, wakati United inacheza na PSG kwenye Ligi ya MabingwaPaul alishangilia kwa nguvu kubwa ushindi wa United ambao uliwaondoa PSG kwenye mashindano hayo.

Ama hakika, Paul Pogba sio maarufu kama anavyosikika. Baadhi ya mashabiki wameenda mbali na kusema kuwa, mchezaji huyu hawezi kuamua matokeo bila kuekewa wachezaji wa kumfichia makosa yake. Vidal, Kante, Pirlo ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuficha makosa mengi ya Paul anapokuwa uwanjani na kwamba United ni sehemu sahihi inayoonesha uwezo halisi wa Paul.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa