Taarifa zinasema kuwa PSG wamewasilisha ofa ya kumsajili Lionel Messi, kwa mujibu wa vyanzo vya TNT Sports Brazil, na pia Mundo Deportivo.

Ripoti zinataja kuwa klabu hii imempa Lionel Mess mkataba wa miaka miwili, na chaguo la kumsajili kwa msimu wa tatu zaidi. Inaaminika kuwa ofa yao haiwezi kufikiwa na Barcelona kwa thamani lakini pia ukiitazama kisoka zaidi.

Uhalisia kuwa PSG walifikia Fainali ya Ligi ya Mabingwa, na sasa wapo kwenye musu fainali kwa msimu huu baada ya kuwaondoa Barcelona kwenye nafasi ya 16 unaonekana kuwapa nafuu zaidi PSG.

Lionel Messi to PSG

Mkataba wa Messi na Barcelona upo ukingoni, na Juni 30 nyota huyu wa miaka 33 atakuwa anamaliza mkataba wake. Mpaka sasa, bado hajaweka wazi maamuzi yake juu ya hatma yake klabuni Barcelona.

Messi anatarajia kufanya maamuzi yake baada ya msimu kuisha, na ni matarajio ya Barcelona kuwa wataweza kumbakiza licha ya ushindani ambao unaibuka kutoka vilabu vingine.

kwa nafasi ambayo amefikia, Messi ndiye anayeweza kufanya maamuzi magumu ya kundoka klabu yake aliyoitumikia mda mrefu au lah. Matarajio ya wengi ni kuwa baada ya sakata lililokwamisha uhamisho wake dirisha lililopita, hatakuwa na hamu ya kusalia Barcelona, lakini hilo halitabiriki ukizingatia namna anmavyojaribu kujitoa kwa timu licha ya yaliyotokea.


 

KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa