Paris Saint-Germain PSG wanatajwa kuwa na uhakika wa kumsainisha nyota Lionel Messi ndani ya wiki mbili na wakapata faida kwenye usajili huo.

Barcelona wamenyosha mikono kuwa masharti ya mishahara ya La Liga yamewashika shati, hivyo hawawezi tena kukamilisha kusaini mkataba mpya na Messi kama ilivyokuwa imekubaliwa awali na pande hizo mbili.

Kwa mujibu wa Sports Mole, baada ya Barca kutangaza kuwa hawawezi kumpa Messi mkataba mwingine, PSG tayari waliamua kufanya tathmini ya uwezekano wa kumsajili staa huyu na pande zote za shilingi kwa faida na changamoto.

Lionel Messii to PSG?

Tathmini ya ndani ya PSG inabainisha kuwa suala hilo linawezekana na linaweza kuwaongeza fedha kwa kuboresha udhamini na biashara kutokana na uwepo wa Lionel Messi.

Mauricio Pochettino, akizungumza na vyombo vya habari amebainisha kuwa dili la kumsaini Messi linawezekana na kwa sasa wanajaribu kufanya tathmini za msingi, amesisitiza kuwa klabu inafanya jitihada juu ya hilo.

PSG wana matumaini kuwa dili la Messi linaweza kuwalipa zaidi, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mauzo ya Jezi.


VUNA MKWANJA NA KASINO ZA MERIDIANBET!

Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa