Wakati ligi soka barani Ulaya zikielekea ukiongoni, maandalizi ya usajili wa dirisha kubwa yameenza kushika hatamu. Wakala ya Erling Haaland- Mino Raiola na baba wa mchezaji huyo – Alf Inge Haaland wameanza kuzunguka nchi mbalimbali.

Kama ilivyokuwa kwa Lionel Messi na Jadon Sancho msimu uliopita, Erling Haaland ameendelea kuteka vichwa vya habari msimu huu baada ya kuendelea kuwa hodari wa kuzifumania nyavu.

Kinda huyu wa Borussia Dortmund ambaye anawindwa na vilabu mbalimbali, anatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya milioni 100. Japokuwa, mkataba wake wa sasa klabuni hapo, unamruhusu kusajiliwa kwa dau la pauni milioni 75 ifikapo 2022 (majira ya joto)

Baba mzazi wa Haaland 0 Alf Inge akiwa na wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola nchini Hispania.

Safari za Mino Raiola na baba mzazi wa Halaand, zinalenga kutaka kujua vilabu vinavyomuhitaji mchezaji huyo vinamipango gani ambayo itakuwa na faida katika maisha ya soka ya mchezaji huyo.

Baada ya Raiola na Inge kutoka nchini Hispania ambapo imeripotiwa kuwa alizungumza na Barcelona pamoja na Real Madrid, wawili hao wanatarajiwa kutua Uingereza ambapo ni vilabu vinne tu (Man United, Man City, Liverpool na Chelsea) ndivyo vinavyoonekana kuwa na uwezo wa kumsajili Haaland msimu huu.

Hakika vita ya kumsajili Haaland inaendelea kupamba moto. Swali ni Je, Haaland ataondoka BVB msimu huu au itakuwa kama habari za Lionel Messi na Jadon Sancho msimu uliopita? Klabu gani itashinda vita hii? Je, atafanikiwa zaidi akiwa nje ya BVB?


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa