Taarifa rasmi kutoka Real Madrid zinaeleza kuwa Nahodha wa timu hiyo Sergio Ramos atakosa michezo yote miwili ya robo fainali ya Ligi Ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool pamoja na El Classico baadae mwezi huu. 

Ramos alipata majeraha misuli ambayo yanatarajiwa kumuweka nje kwa muda wa mwezi mmoja. Ramos alipata majeraha hayo alipokuwa kwenye majukumu ya kimataifa na timu yake Uhispania.

Hili litakuwa pigo kubwa kwa Real Madrid ambao wanategemea sana uwezo wa nahodha wao ambaye amekuwa chachu ya maendeleo ya Klabu hiyo.

Ikumbukwe Ramos alimchezea faulo mbaya sana Salah mchezo wa fainali mwaka 2018 huko Kiev. Katika fainali hizo Salah alilazimika kutoka kipindi cha kwanza cha mchezo huo. Hivi karibuni Mohamed Salah alisema hana kisasi chochote kuelekea robo fainali yao dhidi ya Madrid.

Katika gazeti la Marca, Sergio alisema kwamba anajisikia vibaya sana kukosa michezo hiyo, hasa ukweli kwamba hizi ni mechi ambazo zinamuhitaji sana.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

ramos, Ramos  Kuwakosa Liverpool na El Classico, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa