Lionel Messi hatocheza mchezo mwingine akiwa na jezi ya Barcelona! Licha ya juhudi zilizofanywa na klabu, haikuwezekana kufikia makubaliano ya kumbakisha staa huyo Muargentina huko Camp Nou.

Rasmi: Messi Kuondoka Barcelona

Barcelona ilitangaza kwamba klabu hiyo haitaweza kumbakisha Messi huko Campo Nou, na Muargentina huyo atatakiwa kuondoka baada ya kujiunga na The Blaugrana akiwa na miaka 13.

Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo siku ya Alhamisi jioni, Barcelona iliweka wazi kuwa pande hizo mbili zimefikia makubaliano juu ya masharti ya kifedha na kuongeza mkataba, lakini sheria za kiuchumi na kimuundo zilizowekwa na LaLiga katika kudhibiti hali ya uchumi zimefanya hali hii mbaya kuwa kweli.

“Licha ya kufikia makubaliano kati ya FC Barcelona na Leo Messi, kwa nia wazi ya pande zote mbili kutia saini kandarasi mpya, haiwezi kurasimishwa kwa sababu ya vikwazo vya kiuchumi na kimuundo,” ilisema taarifa hiyo.

Lionel Messi sasa ataendelea kuwa kama mchezaji huru hadi atakapopata klabu ya kusaini kabla ya msimu wa 2021/22.


VUNA MKWANJA NA KASINO ZA MERIDIANBET!

Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa