Rebecca Welch awa mwamuzi wa kwanza mwanamke kuamua mchezo katika ligi ya Uingereza, akichezesha mchezo wa EFL kati ya Port Vale na Herrogate Town.

Katika mchezo huo Port Vale walishinda 2-0, baada ya mechi hiyo kocha wa timu ya Herrogate Town alisema mwamuzi huyo alifanya kazi kubwa licha ya timu yake kupoteza.
MWAMUZI, Mwamuzi Wa Kwanza Mwanamke Ligi Ya Uingereza, Meridianbet
Rebecca akichezesha mechi hiyo ya EFL

Rebecca ana miaka 27, na yupo kwenye orodha ya waamuzi wa FIFA akiwahi kuchezesha mchezo wa fainali ya Kombe la FA la wanawake mwaka 2017 na 2020.

Watu wengi wamechukulia kitendo hicho kama mazingira mazuri ya kuwaona waamuzi wengi wa kike wakichezesha mechi kubwa za ligi za wanaume za Uingereza.

Waamuzi wengi wa kike wamekuwa wakichezesha mechi ndogo ndogo za wanaume na ligi za wanawake. Na wale waliofanikiwa kuchezesha mechi za ligi za wanaume wamekuwa wakihusianishwa na mambo ya udhalilishaji.

Stephanie Frappart alikuwa mwanamke wa kwanza kuchezesha mechi ya kufuzu kombe la dunia kati ya Uholanzi na Latvia lakini haijawahi kutokea mwamuzi wa kike kuchezesha mechi ya ligi ya wanaume ya Uingereza.

Stephanie Frappart mwamuzi mwingine wa kike
Stephanie Frappart mwamuzi mwingine wa kike

Mwamuzi mkongwe Mark Clattenburg anaamini kitendo cha Rebbeca kupata nafasi hiyo kutatengeneza mazingira mazuri kwa waamuzi wa kike wengi zaidi kuchezesha mechi za wanaume.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

MWAMUZI, Mwamuzi Wa Kwanza Mwanamke Ligi Ya Uingereza, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa