Kunako soka la Amerika Kusini, unapozungumzika mashindano ya Copa Libertadores ni kama unaongelea Ligi ya Mabingwa Ulaya, River Plate yaonesha maajabu.

Baada ya takribani wachezaji 20 kukutwa na maambukizi ya Covid19, klabu ya River Plate ilijikuta ikisalia na wachezaji 11 pekee walioruhusiwa kucheza mchezo dhidi ya Independiente Santa Fe.

Sekeseke hili lilishika hatamu pale ambapo magolikipa wote wanne wa kikosi cha kwanza cha Plate walikutwa na maambukizi ya Covid19 huku ombi la kuongeza makipa wawili likikataliwa na hivyo kiungo mkongwe, Enzo Perez (miaka 35) kuchukua jukumu la kulinda mlango.

River Plate, River Plate, Enzo Perez Aonesha Uwezo Golini., Meridianbet
Enzo Perez akionesha uwezo wake golini.

Hakika mwenye nacho hutunzwa, japokuwa Perez sio hodari golini lakini alitumia mbinu zake za kupiga penati kama sehemu ya kujiweka mchezoni na kuuzingatia zaidi mpira usiingie langoni kwake.

Dakika 90 zinamalizika, River Plate 2, Independiente Santa Fe 1. Ushindi dhidi ya miamba ya soka la Colombia, unawaweka Plate kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi lao katika mashindano hayo makubwa kwenye soka barani America Kusini.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

River Plate, River Plate, Enzo Perez Aonesha Uwezo Golini., MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa