Hali sio shwari kwa mshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya Taifa ya Poland, Robert Lewandowski. Hii ni baada ya mchezaji huyo kupata majeruhi ya goti akiwa na timu ya taifa.

Licha ya kupachika magoli mawili katika ushindi wa magoli 3-0 kwenye mchezo dhidi ya Andorra, Lewandowski aliumia goti lake la kulia.

Taarifa rasmi iliyotolewa na shirikisho la soka la Poland imeripoti kuwa, Robert Lewandowski ataukosa mchezo dhidi ya Uingereza (jumatano hii) ikiwa kama hatua ya tahadhari. Badala yake, Lewandowski atarejea Ujerumani ili kupatiwa matibabu ambayo huwenda yakachukua siku 5-10.

Robert Lewandowski, Robert Lewandowski Kurejea Bayern Munich., Meridianbet
Hansi Flick (kushoto) akiteta jambo na Lewandowski (kulia)

Taarifa hii huenda ikawa ni mbaya kwa kocha wa Bayern Munich, Hansi Flick wakati huu ambao timu yake inakwenda kucheza michezo migumu na ya muhimu kwenye kalenda yao.

Bayern watachuana na RB Leipzig (Aprili 3) kabla ya kuwavaa PSG (Aprili 7) katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa.

Baada ya PSG, Bayern Munich watachuana na Union Berlin (Aprili 10) na kisha kumalizana na PSG (Aprili 13). Kwa msimu huu pekee,  Robert Lewandowski ameshapachika magoli 42 na kutoa pasi 8 za magoli kwenye michezo 36 aliyoitumikia Bayern Munich kwenye mashindano yote.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Robert Lewandowski, Robert Lewandowski Kurejea Bayern Munich., Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa