Baada ya kupata ajali kunako mbio za Bahrain Grand Prix 2020, dereva Romain Grosjean anatarajia kurejea tena kwenye mashindano ya Formula 1 mwezi ujao.

Grosjean alipata ajali mbaya kwenye mashindano ya Bahrain GP, 2020 baada ya gari lake kulipuka na kuteketea kwa moto muda mfupi baada ya kufanikiwa kujiokoa kwenye ajali ile.

Ilikuwa ni moja ya ajali mbaya kutokea kwenye mchezo wa F1 na wengi walishangazwa na uwezo wa Romain Grosjean ambaye afanikiwa kuchomoka ndani ya gari huku likiwa linateketea kwa moto.

Wachezaji na wadau mbalimbali wa mchezo wa Formula 1, walimtumia salamu za pole Grosjean muda wote alipokuwa hospitali na sasa, anatarajia kurudi tena kwenye usukani safari hii akifanya mbio ya maonesho akitumia gari la bingwa wa F1 na mchezaji wa timu ya Mercedes – Lewis Hamilton kwenye mbio za French GP 2021, mwezi ujao.

Romain Grosjean, Romain Grosjean Kurejea Kwenye F1 June 2021., Meridianbet
Grosjean (kulia) katika jitihada za kujiokoa kwenye ajali ya gari lake kulipuka.

“Sikutaka kumalizwa kwenye ajali ile. Nilipokuwa hospitali, nilisoma mahali kuwa Toto Wolf (mkurugenzi wa timu ya Mercedes) angefurahi kunipatia siku moja kwenye gari ya F1 kama ningeweza kurejea mchezoni.

“Wakati nilipokuwa kitandani ninamaumivu hospitalini, nilifarijika na ninashukuru kwa fursa hii. Ni nadra sana kupata nafasi ya kuendesha gari la bingwa wa F1 kwa kujifurahisha tu – itapendeza sana” alisema Grosjean.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Romain Grosjean, Romain Grosjean Kurejea Kwenye F1 June 2021., Meridianbet

SOMA ZAIDI

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa