Baada ya kutangazwa kuwa balozi wa Livescore ulimwenguni hapo jana, nguli wa soka, Christiano Ronaldo ameibuka na kueleza kuwa kuna ugumu kuchagua wachezaji watakaokuja kuwa bora kama yeye na Messi lakini anawaona mbali sana Haaland na Mbappe.

Siku ya jana ilikuwa na uzito mkubwa sana kwa wadau wa soka, hususan mashabiki wa Ronaldo baada ya nguli huyo wa soka kuingia mkataba na Livescore na yeye kuwa balozi rasmi kwa misimu miwili mfulululizo. Mkataba huu utampa uhuru Christiano kuwa kwenye matangazo ya Livescore na kuongeza maudhui bora zaidi.

ronaldo
Ronaldo amesaini mkataba na Livescore na atakuwa balozi wao mpaka mwisho wa kombe la dunia 2022

Ingawa kuna watu wachache watapinga ukweli kwamba Ronaldo anashikilia nafasi miongoni mwa wachezaji bora sana duniani. Ila ukweli utabaki kuwa licha ya umri wake wa miaka 36, mchezaji huyu amefanikiwa kushinda mataji akiwa Uingereza, Spain na Italia, lakini pia amesaidia timu yake ya Ureno kushinda Euro 2016 na kushinda tuzo 5 za Ballon d’Or.

Lakini licha ya ukubwa na mafanikio yake, Ronaldo ataendelea kufanananishwa na mchezaji wa Barcelona Lionel Messi, hususan kipindi ambacho cr7 alikuwa akichezea mahasimu wa Barcs, Real Madrid.
Ronaldo na messi wameshinda ballon d'Or 11 kati ya 12
Ronaldo na messi wameshinda ballon d’Or 11 kati ya 12

Wachezaji hawa wawili wamekuwa wakionesha makali yao kwa muongo mmoja sasa, wakishinda mataji mbalimbali, kukusanya tuzo na kuongoza mataifa yao kwenye mashindano mbalimbali. Ila ukubwa wao wanakaribia kwenda mwisho na dunia bado inawaza nani anaweza kuwa ‘Messi ajaye’ au ‘Ronaldo ajaye’?

Baada ya kuhojiwa na kituo kimoja cha televisheni, Christiano alieleza kuwa ni vigumu sana kutaja moja kwa moja nani anaweza kuja kuwa mchezaji bora hapo baadae lakini Kylian Mbappe na Erling Haaland ni wachezaji ambao hana mashaka nao kuhusu kuja kuwa bora sana baadae.

Ronaldo ataja wawili watakaoteka dunia

Erling Haaland amekuwa akihusishwa na vilabu vikubwa, na akiwa katika timu ya Dortmund ameshafanya makubwa sana hivyo bila shaka, kuna makubwa zaidi yanakuja mbele kwa kijana huyu.

Ronaldo ataja
Mbappe amekuwa poa sana toka awe na Neymar

Kwa Upande wa Mbappe pengine ameanza kupata ukubwa mapema, akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa amefanikiwa kuchukua kombe la dunia tayari huku wenzake CR7 na Messi wakishindwa kufanya hivyo. Dunia ipo tayari kushuhudiwa ukubwa wa wachezaji hawa ambao watakuja kuteka soka la dunia na kufanya soka lipendeze kila mtazamaji.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Ronaldo, Ronaldo Ataja 2 Watakaotawala Soka Baadae, MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa