Juventus wanaripotiwa wanajiandaa kuipatia Manchester United nafasi ya kumsaini Paulo Dybala au Cristiano Ronaldo kama sehemu ya makubaliano ambayo yangemfanya Paul Pogba arejee Turin.

Mkataba wa Pogba huko Old Trafford unamalizika Juni mwakani, na nyota huyo wa Ufaransa hivi karibuni alikataa kwamba anafanya mazungumzo na mabingwa hao wa Uingereza wa mara 20 juu ya mkataba mpya.

Ronaldo na Dybala
Ronaldo na Dybala

Kwa mujibu wa Tuttosport, bosi wa Juve anayerejea Massimiliano Allegri anatamani sana mshindi huyo wa Kombe la Dunia arejee kwa miamba wa Italia katika msimu huu wa uhamisho.

Taarifa zinadai kwamba Juve yuko tayari kumtoa Dybala au Ronaldo kuongeza uzito katika dili lao na Pogba, huku wachezaji wote wakiwa wanahusishwa na kuondoka Juventus katika soko hili la uhamisho.

Paul Pogba and Ole Gunnar Solskjaer
Paul Pogba anahusishwa na dili la mabadilishano kwenda Juventus na Ronaldo au Dybala

Ronaldo anafikiriwa kuwa na wazo la kurudi Man United msimu huu wa joto, wakati Dybala pia hapo awali alikuwa akihusishwa na kuungana na Ole Gunnar Solskjaer.

Pogba, atakuwa huru kuingia kwenye mazungumzo ya kandarasi na vilabu vya kigeni mnamo Januari 2022, na Real Madrid, Barcelona na Paris Saint-Germain wote wanasemekana kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mka taba wake.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa