MADRID, HISPANIA. Gwiji la soka la Brazil, Ronaldo Nazario ameomba radhi kwa staili yake ya nywele aliyoisema kuwa ya hovyo aliyonyoa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2002 na kuwaomba wamama wa watoto zao ambao waliiga mtindo huo wamsamehe.

Straika huyo wa zamani wa Inter Milan na Real Madrid, Ronaldo bado anakumbukwa na staili yake hiyo ya nywele, ambapo alinyoa kipara kote na kubakiza pembetatu juu ya paji la uso, mtindo ambao mwenyewe alidai alibuni ili kuwafanya watu kusahau kwamba yeye ni majeruhi na kuzungumzia nywele zake kwenye fainali hizo.

Ronaldo, 44, ambaye kwa sasa ni rais wa klabu ya Valladolid inayocheza La Liga, ameelezea staili yake hiyo ya nywele kuwa ya hovyo kabisa wakati alipofanyiwa mahojiano na Sports Illustrated.

 

Ronaldo, Ronaldo Awaomba Radhi Kina Mama Duniani., Meridianbet

Staa huyo aliyewahi kuichezea pia Barcelona alisema kwamba alinyoa mtindo huo ili kuwafanya waandishi wa habari wa Kibrazili kusahau kuzungumzia maumivu yake ya misuli ya mguu aliyopata kabla ya mechi ya nusu fainali dhidi ya Uturuki ili kumfanya kuwekeza akili yake kwenye mechi, ambapo alifunga bao na kuifikisha Brazil fainali.

Ronaldo alisema: “Nawaomba radhi mama wote ambao watoto wao waliiga kwa kukata nywele zao mtindo nilionyoa. Niliponyoa staili ile, wachezaji wenzangu waliniuliza, ‘Umeipenda?’ Walisema, ‘Hapana, ni ya hovyo! Nyoa nywele zote!’. Lakini, waandishi wa habari waliona staili ya nywele na kusahau habari za majeruhi.”

Ronaldo, anahesabika kama mmoja wa mastraika bora kabisa kwenye historia ya soka na alisema jina lake amepewa baada ya daktari aliyemzalisha mama yake katika hospitali moja huko Rio de Janeiro.

 

Ronaldo, Ronaldo Awaomba Radhi Kina Mama Duniani., Meridianbet

“Daktari alimzalisha mama yangu bure kwa sababu wazazi wangu hawakuwa na uwezo wa kulipia gharama.

“Mama yangu alimpelekea kilo tatu za dagaa kamba aliokuwa amewavua, kisha wazazi wangu wakaamua kuniita jina la daktari huyo.

Ronaldo, ambaye ni baba wa watoto wanne, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuongezeka uzito tangu alipostaafu soka Februari 2011, lakini alidai kwamba atarudi uwanjani kucheza kama uzito utapungua.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Ronaldo, Ronaldo Awaomba Radhi Kina Mama Duniani., Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa