Kijijini kabisa huko Sedhiou Senegal, alizaliwa na kukua kwenye umaskini wa kiwango cha juu. Kwa Sadio Mane umaskini si hadithi aliyoisoma kwenye kitabu, si tukio alilolitazama kwenye filamu.

Kwa Sadio Mane, umaskini ulikuwa ndugu yake wa karibu aliyelala nae kitanda kimoja, akaamka asubuhi na kunywa nae chai kisha akaenda nae mtaani kuzurura. Umaskini ulikuwa sehemu ya maisha yake ya utotoni.

Kwasababu hiyo alicheza na wenzake mitaani, kwenye barabara za vumbi bila viatu. Nyumbani hawakuwa na pesa ya kumnunulia vifaa vya michezo wala kumlipia ada ya kujiunga na academy za soka.

Siku moja akiwa na miaka 15, walisikia juu ya akademi moja inayofanya usahili wa vijana wadogo. Mane akiamini kuwa anaweza, aliishawishi familia yake impeleke akajaribu bahati yake.

Mane

Baada ya ushawishi mkubwa Mjomba wake alijitolea kusafiri nae hadi Dakar ilipokuwepo hiyo akademi. Wakasafiri zaidi ya maili 500 kutoka kijijini kwao hadi mji mkuu Dakar.

Walipofika huko walikuta watoto wengi wakifanyiwa majaribio. Mane alimfuata mzee mmoja aliyekuwa anasimamia lile zoezi na kujieleza.

Yule mzee alimtazama kwa mshangao na kumuambia, “Na wewe umekuja kufanya majaribio?” Mane alimjibu “NDIYO”. Yule mzee akamuambia, “Na hivo viatu vilivochakaa kiasi hicho?? Isitoshe hauna hata bukta ya kuchezea”

Bila uwoga Mane alimuambia, “Hivi ndivyo vifaa bora nilivo navyo. Nisingeweza kupata vingine vizuri zaidi ya hivi.”

Basi yule mzee alimpa nafasi, akamuingiza uwanjani. Mane alipogusa mpira, alipigwa na butwaa. Akamuita nje na kumuambia, “Nakuchukua moja kwa moja. Hauhitaji kuendelea na majaribio”

Hivo ndivyo alivosajiliwa na akademi ya ‘Generation Foot’. Akalazimika kuhamia Dakar. Kwasababu hakuwa na ndugu yoyote huko, mjomba wake alimtafutia familia itakayomlea. Akaishi na watu ambao hawakuwa ndugu zake wala hakuwajua kabla.

Mane
Timu alizopita Mane

Aliishi huko hadi aliposajiliwa na Metz. Na historia yake ilibadilika moja kwa moja. Leo Sadio Mane na familia yake sio wale masikini walioshindwa kununua viatu miaka 20 iliyopita.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

mane, Sadio Mane na Maisha ya Kimaskini, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa