Paris Saint-Germain inaripotiwa kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah msimu huu wa joto ikiwa Kylian Mbappe ataondoka klabuni hapo.

Mbappe bado hajasaini kandarasi mpya na mabingwa hao wa Ufaransa, na mshambuliaji huyo anatarajiwa kuuzwa katika soko lijalo ikiwa hatasaini mkataba mpya.

Real Madrid inaendelea kuhusishwa sana na mshindi huyu wa Kombe la Dunia, ambaye amebakiza zaidi ya miezi 12 kukamilisha mkataba wake wa sasa huko Paris.

Kylian Mbappe
Kylian Mbappe hajasaini mkataba mpya, anatarajuwa kuwa ataondoka PSG.

Kwa mujibu wa Le Parisien, PSG inafanya mipango ya dharura iwapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ataondoka klabuni hapo, na klabu ikimtambua Salah wa Liverpool kama mbadala.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri, ambaye anatajwa kuwavutia Real Madrid na Barcelona, ​​hivi karibuni alibainisha kwamba Liverpool bado hawajajaribu kuzungumza naye juu ya mkataba mpya.

Salah kwa mara nyingine, amekuwa katika kiwango cha kuvutia pale Liverpool msimu huu licha ya panda shuka ya timu hiyo, akifunga mabao 29 katika mechi 46 za mashindano yote, ikiwa ni pamoja na magoli 20 katika michezo 32 ya Ligi Kuu.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Mbappe, Salah Kama Mbadala wa Mbappe PSG, Meridianbet

SOMA ZAIDI

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa