Sam Allardyce au muite “Big Sam” mzee wa kuokoa majahazi yanayozama. Safari hii, mambo yamekuwa tofauti ndani ya klabu ya West Brom Albion.

Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Arsenal, ilithibitika rasmi kuwa West Brom wanashuka daraja na kurejea kwenye ligi ya Championship. Msimu uliopita, The Hawthorns walipanda daraja na kucheza Ligi Kuu [EPL] lakini sasa wanarejea tena walikotoka.

Licha ya klabu hiyo kumuwekea ofa mezani, Sam Allardyce ameamua kuchukua uamuzi wa kutoikubali ofa hiyo na badala yake ataachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Sam Allardyce alichukua mikoba wa Slaven Bilic ambaye alitimuliwa klabuni hapo mwezi Disemba,2020 na alisaini mkataba wa miezi 18. Hii ni mara ya kwanza kwa kocha huyu kushindwa kuokoa jahazi kwa kila timu aliyikuta ikitaabika.

Aliwahi kuifundisha Bolton, Sunderland, West Ham United, Everton, Newcastle United, Crystal Palace na timu ya Taifa ya Uingereza. Taarifa za kuachana na West Brom Albion zimekuja ikiwa ni saa 24 tu zimepita tangu mkongwe Roy Hodgson kutangaza kuachana na soka la EPL akiwa kama kocha wa Crystal Palace.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Sam Allardyce, Sam Allardyce Kuondoka West Brom Msimu Huu., MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa