Winga wa Klabu ya Borussia Dortmund, Jadon Sancho amesema kuwa “anafurahi sana” kushirikiana na wachezaji wachanga wa Klabu hiyo na anataka kusaidia kuwaongoza – Winga huyo wa kimataifa England mwenye umri wa miaka 20, ndiye chaguo la kwanza msimu huu wa joto kusajiliwa na Manchester United.

Lakini Mkurugenzi wa Michezo wa Dortmund, Michael Zorc alisema Jumatatu Sancho ataendelea kusalia kwenye Klabu hiyo ya Ujerumani msimu ujao.

“Ninafuraha na maisha ya hapa,” alisema Sancho baada ya kuanza maandalizi kwa mchezo wa kirafiki Buki nchini Uswisi, wote pamoja na Jude Bellingham na Gio Reyna wenye umri wa miaka 17 wakicheza mechi hiyo.

Sancho, Sancho Afurahia Maisha ya Dortmund, Meridianbet

“Sisi ni kundi maalumu. Tuna wachezaji wachanga maalumu wanaochipukia, Nimefurahia sana kushirikiana nao na kuwaongoza”.

“Nilijiunga nilipokuwa na umri wa miaka 17 – baadhi ya wachezaji wengine wana umri kama huo, Nimekuwa hapa na nimefanya vema. Naweza kuwaongoza katika kile kizuri na kisichosawa kufanya, Naweza kuwahimiza kwa matumaini pia.”

United ni kama wameshindwa Kumsajili kinda huyo wa zamani wa Manchester City, kwani wanadhani dau wanalotaka Dortmund takribani £100m, mshahara wa mchezaji na ada ya wakala yote ni ya juu sana kutokana na athari ya kifedha baada ya janga la COVID-19 – Tarehe 10 Agosti ilikuwa ndio mwisho wa klabu hiyo ya Bundesliga kupokea ofa kuhusu uhamisho wa Sancho.

Sancho, Sancho Afurahia Maisha ya Dortmund, Meridianbet


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma zaidi

35 MAONI

  1. Sancho ni mchezaji anae juwa na hakuna timu ambayo ingemkataa yeye ila kwa sababu yeye anapenda kuendelea Dortmund basi tunaheshimu maamuzi yake

  2. Sancho ni mchezaji mzuri halafu anachokiamini kuwa furaha ndio mafanikio yake hauwezi kuchezea club ambayo hauipendi inamaana utakosa mafanikio kwa kutokipenda kitu nakutakia mafanikio mema

  3. Nadhani Sancho anatakiwa kufikiria mara mbili mbili kuondoka Dortmund iliyomupa nafasi ya kucheza na kujulikana. Coutinho mpaka leo atakuwa anajuta kuondoka Liverpool iliyomupa nafasi ya kucheza na kujulikana kila mahali. Dortmund ndio mahali sahihi kwake kuwepo#meridianbettz

  4. Pesa nyingi sana ambayo wanaitaka kwa Sancho man wanatakiwa kuachana klna Jordan Sancho na kuangalia wachezaji wenye uwenzo mkubwa na wapo kwenye vilabu vidogo vidogo

  5. Nadhani Sancho anatakiwa kufikiria mara mbili mbili kuondoka Dortmund iliyomupa nafasi ya kucheza na kujulikana. Coutinho mpaka leo atakuwa anajuta kuondoka Liverpool iliyomupa nafasi ya kucheza na kujulikana kila mahali. Dortmund ndio mahali sahihi kwake

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa