Jadon Sancho hatokuwa sehemu ya kikosi cha Borussia Dortmund kitakacho menyana na Manchester City kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa kutokana na kutokuwa fit vya kutosha.

Sancho Nje Dhidi ya Man City Licha ya Kuanza Mazoezi

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England alikosa mechi kadhaa mwezi uliopita kwa klabu na zile za kimataifa kutokana na jeraha la paja.

Maendeleo chanya ya kuumwa kwake yalifanya arejee  mazoezini lakini kukutana na timu yake ya zamani imekuwa ni karibu sana.

Bosi Edin Terzic amewaambia maripota katika mkutano na waandishi kabla ya mechi pale alipoulizwa juu ya hali ya Sancho: “Jadon hatokuwa katika timu yetu ingawa ameanza kufanya mazoezi tena nasi.”

“Anafanya kila linalowezekana ili aweze kurejea mchezoni tena na tungependa tuwe naye siku ya kesho lakini hawezi.

Dortmund wanarejea katika mchezo wa Champions League wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha 2-1 katika dimba la Etihad Stadium mechi ya kwanza ya robo fainali.

Uwepo wa Sancho ungeongeza nguvu kwa timu ya Dortmund ambao wamekuwa wakisuasua msimu huu huku wakikaa katika nafasi ya sita katika msimamo wa Bundesliga.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

Sancho, Sancho Nje Dhidi ya Man City Licha ya Kuanza Mazoezi, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa