Wachezaji wa ligi kuu nchini Italia Serie A wanaweza kurejea mazoezini kuanzia Mei 4 mwaka huu kwa mazoezi ya mmoja mmoja na Mei 18 kwa mazoezi ya timu.

Hatua hiyo inatokana na serikali nchini humo kutangaza hatua za kuanza kulegeza masharti ya marufuku ya kutoka nje (lockdown), iliyopo sasa kutokana na janga la virusi vya Corona.

Kuna dalili kuwa huenda ligi kuu ya Italia ikarejea kati ya Mei 27 na Juni 2 mwaka huu ili msimu umalizike mwanzoni mwa mwezi Agosti, licha ya kutokuwepo kwa taarifa rasmi kuhusu kurejea kwa ligi hiyo.

, Serie A Kurejea Mei 27?, Meridianbet

Shirikisho la Soka nchini Italia (FIGC) limeanza mpango madhubuti wa kuwapima maambukizi ya virusi vya corona wachezaji pamoja na maafisa wengine wanaohusika, ambapo kila timu itapewa vifaa maalum vya kufanyia vipimo hivyo.

Utaratibu wa mazoezi utakuwaje? Kwa kuanzia, kila timu itaunda kikundi cha wachezaji wachache wakiwa na mtaalam wa ufundi, daktari na mtaalamu wa viungo, kisha kila kikundi kitajitenga katika kambi ndogondogo na kuendelea mazoezi.

Hadi jana nchini Italia kumeripotiwa vifo 26,644 vilivyotokana na ugonjwa wa COVID 19 ikiwa ndiyo kinara barani Ulaya kwa idadi ya vifo, na kwa jana Jumapili vimeripotiwa vifo 260 pekee ikiwa ni idadi ndogo zaidi ya vifo kwa siku tangu Machi 14 mwaka huu.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa