AC Milan: Mikataba ya Watatu, Kizungumkuti.

Watoto wa mjini sikuizi wanatumia msemo wa “kumekucha” kwa minajili hii, AC Milan kumekucha! Wachezaji watatu wanaendelea kuumiza vichwa viongozi kuhusu mikataba yao.

Mabosi wa San Siro bado wapo kwenye mazungumzo yanayoenda mbele na kurudi nyuma linapokuja suala la mikataba ya wachezaji watatu ambao ni mihimili ya timu hiyo.

Imeripotiwa kuwa, kiungo mshambuliaji – Hakan Calhanoglu, golikipa – Gianluigi Donnarumma na mshambuliaji mkongwe – Zlatan Ibrahimovic, wote wanamaliza mikataba yao na AC Milan mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mafanikio waliyonayo mpaka sasa msimu huu, timu hiyo inawategemea zaidi wachezaji hawa katika ujenzi mpya wa kuirejesha klabu hiyo kwenye ubora wake. Milan kwa sasa wanashika nafasi ya 2 nyuma ya majirani zao – Inter kwenye msimamo wa Serie A wakiwa na mchezo mmoja zaidi ya Inter.

Hakan Calhanoglu

Kulingana na Sky Italia, imeripotiwa kuwa mazungumzo kati ya Milan na Calhanoglu yamegonga mwamba. Hii ni kutokana na mchezaji huyu kutaka mshahara mnono kama uongozi wa klabu hiyo unamtaka asaini mkataba mpya.

Sambamba na majadiliano kuwa magumu, vyombo vya habari vimeenda mbali zaidi na kuripoti kuwa, Juve inamtizama kiungo huyu na huenda wakamsajili kama mchezaji huru, mwishoni mwa msimu huu.

Kwa Donnarumma imeripotiwa kuwa maongezi ya kuongeza mkataba wa golikipa huyu kinda (miaka 21) yameanza na pande zote mbili (uongozi pamoja na mchezaji) zinamatumaini, muafaka utafikiwa kabla ya msimu huu kuisha.

Ibrahimovic (kushoto) akiwa na Donnarumma (kulia).

Waswahili husema ‘utu uzima dawa’. Hii ndio hali ilivyo kwa Zlatan Ibrahimovic, yeye ameweka wazi lengo lake la kuendelea kubaki San Siro kwa msimu mmoja zaidi.

Ikumbukwe kuwa, Zlatan alisaini mkataba wa msimu mmoja pekee na kama hatoongezewa mkataba, atakua mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.

Kwa habari zilivyo, inasemakana mkataba mpya wa Zlatan hautobadilika chochote zaidi ya kuongezwa mwaka mmoja mbele na ndani ya siku 7-10 zijazo, Zlatan anaweza kusaini mkataba mpya na AC Milan.

AC Milan wataweza kuwabakiza Zlatan, Calhanoglu na Donnarumma au ndio watapungiana mikono ya kwa kheri mwishoni mwa msimu huu?


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

5 Komentara

    Mwenye kisu kikali Ndiye anakula yama

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Habarii Moto motoo

    Jibu

    Wafanye kumaliza hiyo hali

    Jibu

    Kaz ipo

    Jibu

Acha ujumbe