Kiungo wa Juventus Adrien Rabiot ameripotiwa kuibuka kwenye rada za Chelsea kuelekea dirisha la uhamisho la msimu ujao wa joto.

Nyota huyu wa miaka 25 amecheza kwenye mechi 72 tangia alipowasili Turin kama mchezaji huru akitokea Paris Saint-Germain mwaka 2019.

Hata hivyo, wakati Juventus wakiwa kwenye mpango wa kupunguza mzigo wao wa mishahara ya wachezaji, staa huyu amekuwa akihusishwa zaidi na kuondoka klabuni hapo.

Kwa mujibu wa Tuttomercato, Chelsea watatumia nafuu ya hali hii kujaribu kuwasilisha ofa yao ya kumsajili Rabiot.

adrien rabiot juventus

Licha ya ukweli kuwa ana uhakika wa wachezaji kwa safu ya kati, Thomas Tuchel anaweza kutarajia kufanya mabadiliko kidogo kupitia dirisha lijalo, na hii itakuwa ni moja ya fursa muhimu kwake ikiwa anataka Rabiot abadilishe hali ya hewa kwenye safu ya kati.

Kwa mujibu wa ripoti, Chelsea wanaunga tela kwa Everton na Manchester United ambao kwa pamoja wanatajwa kuwa wapo kwenye mbio za kuiwania saini ya staa huyo.


 

INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

Rabiot, Adrien Rabiot Kwenye Rada za Chelsea, Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa