Ciro Immobile Akaribia Rekodi ya Ufungaji Ulaya.


Matumaini ya Cristiano Ronaldo kuibuka mfungaji bora mbele ya Ciro Immobile katika soka ya Bara Ulaya msimu huu yanazidi kupotea, baada ya kushindwa kutikisa nyavu za wapinzani katika mchuano ulioshuhudia waajiri wake Juventus wakichapwa 2-0 na Cagliari.

Nyota huyo matata mzawa wa Ureno anajivunia mabao 31 kutokana na kampeni za Ligi Kuu ya Italia (Serie A) hadi kufikia sasa msimu huu.

 

Ciro Immobile Akaribia Rekodi ya Ufungaji Ulaya.

Licha ya Juventus kuonekana kutamalaki mechi na kuwazidi maarifa wapinzani wao katika takriba kila idara, ni Cagliari ndio waliotumia vyema uwanja wao wa nyumbani na kuvuna ushindi muhimu.

Mabao ya kikosi hicho yalifumwa wavuni na Luca Gagliano na Giovanni Simeone katika dakika ya 8 na 45 mtawalia.

Ronaldo kwa sasa anahitaji mabao manne zaidi ili kumfikia Ciro Immobile wa Lazio katika vita vya kuwania taji la mfungaji bora miongoni mwa wanasoka wote wa ligi za bara Ulaya msimu huu.

Immobile alifunga bao lake la 35 msimu huu mnamo Jumatano ya Julai 29 katika mechi iliyowashuhudia Lazio wakiwapepeta Brescia 2-0.

 

Ciro Immobile Akaribia Rekodi ya Ufungaji Ulaya.
 

Ikisalia mechi moja pekee kabla ya kampeni za Serie A kutamatika rasmi msimu huu, Immobile ndiye anapigiwa upatu kuibuka mfungaji bora wa bara Ulaya.

Bao lake la hivi karibuni lilimwezesha kumpiku Robert Lewandowski wa Bayern Munich aliyefunga rasmi kampeni za Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) kwa magoli 34.

Immobile kwa sasa anasalia na bao moja pekee kufikia rekodi ya Gonzalo Higuain aliyewahi kufunga idadi kubwa zaidi ya mabao katika msimu mmoja wa Serie A.

Higuain alipachika wavuni mabao 36 akivalia jezi za Napoli mnamo 2015-16.


Nini kinachokupa raha kama michezo ya kasino ya mtandaoni? Hasa unapojua kuwa kuna ushindi, jackpot na mizunguko kibao ya bure.
Ungana na bwana Meridian kupata ushindi na burudani.

Cheza Hapa Sasa

47 Komentara

    Ciro apambane tu atafika anapopataka#Meridianbettz

    Jibu

    Bado serie A zimabaki mechi mbili kila timu kumaliza msimu, lolote linaweza kutokea. Pamoja na mafanikio ya Ciro Immobile,Lewandowsk, Ronaldo na Benzema bahati mbaya msimu huu Ballon D’Or imefutwa#meridianbettz

    Jibu

    Naamini cr7 lazima ataibuka kidedea kufikisha magoli mengi

    Jibu

    Ciro aongeze juhudi
    #meridianbettz

    Jibu

    Bora Ciro awe ndo apewe tuzo isiwe mazoea kila msimu majina ni yale yale yaliyozoeleka

    Jibu

    Ciro aongeze juhudi

    Jibu

    Aongeze juhudi aendelee kukaza Buti atafika malengo

    Jibu

    Navyo mjua Ronaldo akubaligi kushindwa kabisa atafanya afanyavyo mpaka afike pale panapo stairi

    Jibu

    Aendelee kukaza buti atafika malengo#meridianbettz

    Jibu

    Ciro immobile ni mchezaji hanayekuja na kasi ya hajabu sana kila kitu kinawezekana kikubwa hawe na nia tu asikate tamaa

    Jibu

    Ciro Immobile anakuja vizuri

    Jibu

    Ciro akaze buti

    Jibu

    Aongeze juhudi na apende anachokifany!!

    Jibu

    Aongezee bidiii

    Jibu

    Aongeze juhudi tu

    Jibu

    Ciro amaekuwa kwenye kiwango kizuri sana msimu huu hivyo anastahili kutwaa kiatu cha dhahabu cha Italia

    Jibu

    Immobile yuko vizuri Sana na anapokua dimbani hua anajituma Sana lengo lake kuakikisha nyavu za timu pinzani zinatikisika.

    Jibu

    Akuna na washindana na cr7

    Jibu

    Kwa namna hii Rinaldo lazima apigwe bao na ciro

    Jibu

    Ciro ameonyesha kiwango kizuri sasa hvi

    Jibu

    Ciro Immobile ndio atakua kinara wa magoli kwani Ronaldo kwa hii mechi moja iliyobakia hawezi kufikia magoli ya Ciro Immobile

    Jibu

    apamabne zaid

    Jibu

    Habari mzuri

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

    Immo ni mchezaji mahiri eneo la 18 hivyo imemfanya afunge mabao mengi season hii

    Jibu

    Ciro aongeze juhudi aipeke kazi yake na aiheshimu pia atafanya vizuri zaidi

    Jibu

    Pambana tu

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Daah nilikuwa na matumaini na Ronaldo kupata kiatu ila ndio Ciro naye amepambana

    Jibu

    duh ajitahid tu

    Jibu

    Kwa hiyo Cristian Ronaldo ndio amekosa hiyo tuzo da siamin

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Akaze buti tu atapata

    Jibu

    Good

    Jibu

    Akaze buti atafkia malengo

    Jibu

    Aongezee juhud

    Jibu

    Sababu bado mechi moja Kama atakaza kesho atachuku kiatu Cha ufungaji Bora ulayaa

    Jibu

    Japo mechi zimebaki chache ila lolote linaweza tokea

    Jibu

    Ciro immobile amekua na msimu bora sana ndan ya kikosi cha lazio

    Jibu

    Maoni:Habari njema

    Jibu

    Hapo wote wakal game ya mwixho ndo itahamuan nan mshindi

    Jibu

    Safiii

    Jibu

    ajitahidi atafikia malengo lakini sidhani kama Christian Ronald anaweza mwachia iv iv

    Jibu

    Wanashindan kwer

    Jibu

    Wakomae

    Jibu

    Cr7 msimu huu hana bahati

    Jibu

    Hongera yake Ciro mana kapata

    Jibu

Acha ujumbe