Klabu ya Juventus imeripotiwa kufungua mazungumzo na mchezaji wake ambaye yupo kwa mkopo kwenye klabu ya Rangers Aaron Ramsey ya kutaka kuvunja nae mkataba mapema mwaka huu kabla ya majira ya kiangazi.
Aaron Ramsey ambaye alijiunga na klabu ya Rangers kwa mkopo akitokea juventus mwezi January, amekuwa akizungumzwa vibaya siku za karibuni baada ya kukosa mkwaju wa penati kwenye mchezo wa fainali ya Europa League dhidi ya Eintracht Frankfurt. Huku pia kukiwa na taarifa kuwa Ranger hawana mpango wa kumnunua moja kwa moja kwa ajiri ya msimu ujao.
Kutokana na majeraha ya mara kwa mara yalimfanya asiweze kucheza mara nyingi kwenye klabu ya Juventus na wimbi hilo alikwenda nalo kwenye kikosi cha Ibrox na kumfanya aweze kuanza kwenye michezo tisa pekee kwenye mashindano yote.
Juventus wamepanga kumuachia huru kuweza kupunguza mzigo wa bill za mshahara wake ili waweze kuingia tena sokoni kupata wachezaji ambao wataweza kuboresha kikosi cha kwa msimu ujao.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.