Kocha wa Juventus – Andre Pirlo, hanashaka na namna timu yake inavyofanya usajili. Kwake, anasisitiza kwamba wanajua namna gani wanashughulika na usajili kama timu.

Taarifa mbalimbali za vyombo vya habari zinasema Juventus wapombioni  kukamilisha usajili wa Feredico Chiesa kutoka Fiorentina.

Pamoja na usajili huo, kikosi cha Pirlo huwenda kikawapunguza baadhi ya wachezaji. Sami Khedira, Mattia De Sciglio na Douglas Costa ni kati ya wachezaji wanaohusishwa na kutimka kwenye kikosi cha Juventus.

Pirlo anasema muda ukifika kila kitu kitajulikana, kama kuna mtu atasajiliwa ama kuondoka, tusubiri mpaka dirisha lifungwe – Jumatatu usiku.

“Kama kuna yeyote atafika, tutamuona jumatatu jioni. Mkurugenzi wa michezo – Fabio Paratici anashughulikia hilo, tunajua tunachokifanya.

Khedira, De Sciglio and Douglas Costa wote wanaendelea na mazoezi kama wachezaji wengine na wanaweza kucheza.

Kuelekea mchezo wao dhidi ya Napoli, Pirlo amenukuliwa akisema “ninaamini Napoli kwa ujio wa Gattuso, wamebadilisha mtizamo.”

Mpaka sasa, Juventus wamefanya usajili mmoja, Arthur ametoka Barcelona na kujiunga na Juventus. Miralem Pjanic akajiunga na Barcelona akitokea Juventus.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

34 MAONI

  1. Juventus kwanza bado wanakikosi kipana na cha ushindani Pirlo anakazi moja tuu kuhakikisha vijana wanaelewa Falsafa yake tuu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa