Nyota wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Juventus Paul Pogba leo kupitia mitandao yake ya kijamii amaechapisha video ya kuthibitisha kufanyiwa upasuaji na baada ya kusumbuliwa na jeraha la goti kwa wiki kidhaa sasa.

Pogba mwenye miaka 29, alipata majeraha ya goti akiwa nchini Marekani kwenye michezo ya Pre-season, na awali ilibidi afanyiwe upasuaji nchini Marekani kabla ya klabu hiyo kuamua kumtafutia mshauri wa afya wa kuangalia ni namna gani atafanyiwa upasuaji ili aweze pona haraka.

Pogba, Pogba Athibitisha Kufanikiwa kwa Upasuaji Wake, Meridianbet

Awali alikutana mshauri nchini Ufarasana kwa ajiri kuangalia uwezekano wa uchaguzi upi bora kwa ajiri ya upasuaji wake huku kukiwa njia mbili za kuweza kutibu jeraha lake ambapo awali ni kuponya kidona na ya pili ndio upasuaji wa kuaondoa “meniscus”.

“Natumai nyote mko vizuri, mimi ni mzima na mshukuru mungu upasuaji umenda vizuri. Natarajia kurudi hivi karibuni, ningependa kuwashukuru ninyi nyote kwa jumbe zenu, hamasa yenu na kujua kwamba niko sawa kiakili licha mashaka yote na majeraha.

“Pamoja na matatizo yote nainua kichwa changu juu, sipo peke yangu nipo na mungu wangu wangu, nyote nawashukuru jumbe zenu zote, ushirikiano wenu wote ambao nimeouna kwenye mitandao ya kijamii.

“Tutarudi kwa kishindo hivi karibuni na natumai itakuwa sawa natuma salamu zangu kwenu na kuwaaga.” Alichapisaha video kwenye mtandao wa Twitter


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa