Pogba Rudi Juventus Uwe na Furaha Tena

Kiungo wa zamani wa Juventus, Claudio Marchisio alimwambia nyota wa Manchester United Paul Pogba arudi kwa miamba wa Serie A ili aweze “kufurahi tena”.

Pogba amekuwa akihusishwa na kuondoka United, ambako alirudi akitokea Juve mnamo 2016.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alizua uvumi mpya juu ya hatma yake ya baadaye alipozungumzia furaha yake kuwa katika jukumu la kimataifa, akisema “Timu ya kitaifa ya Ufaransa ni pumzi ya hewa safi”.

Kwa wanaoweza kudadavua wanaona anasema kama ni kama amepata mapumziko kidogo kutoka kwenye heka heka za Man United.

Paul Pogba
Kwa pogba, kwenda kuitumikia timu yake ya taifa ni kupata nafasi ya kupumua kidogo toka United

Pogba ameripotiwa kuwindwa na miamba ya Juventus na LaLiga Real Madrid, na mwenzake wa zamani wa timu hiyo Marisio angependa kumwona amerudi Turin.

Akijibu tweet kutoka kwa Pogba, Marchisio aliandika: “Tafadhali @paulpogba. Njoo kwa @ juventusfc… utafurahi tena. Mimi pia #tilltheend (mpaka mwisho)”

Nyota huyu alikuwepo kwa misimu minne huko Juventus kati ya mwaka 2012 na 2016, akishinda Serie A katika msimu hiyo yote, na Mataji mawili ya Coppa Italia na taji mataji mengine mawili ya Supercoppa Italiana.

Mshindi huyu wa Kombe la Dunia 2018 ameshinda Kombe la EFL na Ligi ya Uropa tangu arejee United.

Pogba amecheza mechi saba za Ligi ya Premia akiwa na United msimu huu, huku kikosi ca Ole Gunnar Solskjaer kikiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.

Yeye hana bao wala asisti kwenye ligi msimu huu, wakati pasi zake kamilifu zikiwa ni asilimia 79.9, ikiwa ni kiwango cha chini kabisa tangu alipowasili United.

Marchisio anaamini staa huyu akirejea Juventus basi atarejea kuwa na furaha tena anapokuwa uwanjani.


 

BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

22 Komentara

    Nice update

    Jibu

    Keel pogba rudi juventus kumenoga hasaivi

    Jibu

    pogba akiondoka united watapata pigo kubwa sana

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Pogba bora arud juve tu

    Jibu

    Pogba maisha ndani ya united yamefikiah tamati hv ni visa tu

    Jibu

    Pogba bora urudi Juventus

    Jibu

    Sizani ila Pogba Man U anayo moyoni atakama akiludi juve haliipenda tangia kitambo Sasa nichangamoto tuu kwenye krabu kilakitu nisubila namipango

    Jibu

    Pogba achague wap mahar sahihi kwake

    Jibu

    Uamuzi ni wake, yetu macho.

    Jibu

    Salam zao huko aendako

    Jibu

    Pogba kwa mri alio kua nao sasa hanatakiwa alijenge soka lake hipasavyo mda unakwenda kila kitu kinaenda na wakati wachezaji wengi chipukizi wana kuja na kasi ya hajabu na hasipo angalia hanaweza kupoteza mashabiki wake

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Pogba hatakiwi kurudi Juventus kuna timu nyingi sana akienda huenda akashine.

    Jibu

    Inabidi aangalie na upande mwengine

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Pogba atafute tu seheku ya kwenda nina himani yy mchezaji mkubwa vilabu vingi vinamuitaji

    Jibu

    Aende tuu juventus naona kimewaka

    Jibu

    Pogba rudi nyumbani Turin kumenoga

    Jibu

    Pogba akili na mawazo yake yapo madrid ba si juve

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Bora ajiendee zake juventus

    Jibu

Acha ujumbe