Sarri Hakuwaamini Wachezaji wa Juventus

Licha ya kuiongoza Juventus kutwaa ubingwa wa Serie A msimu uliopita, Maurizio Sarri alijikuta akitimuliwa Juventus baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Lyon.

Mengi yalisemwa kutokana na tukio hilo na sasa aliyewahi kuwa mchezaji wa Juventus, Mirallem Pjanic amefunguka na kudai Sarri hakuwaamini wachezaji wake wa Juventus.

Raisi wa Juventus – Andrea Agnelli alinukuliwa akisema kulikuwa na kutoelewana kati ya Sarri na wachezaji nyota wa timu hiyo na hivyo ilibidi mmoja aondoke.

Akizungumza na Tutto Sport, Pjanic ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Juventus chini ya kocha huyo, alinukuliwa akisema ” Sarri hakuwa anawaamini wachezaji wake, na hilo lilinisumbua sana.

“Kila mchezaji kwenye timu ile alikuwa anajitoa kwa ajili ya timu. Unaweza usielewane na mtu mmoja au wawili lakini muda mwingine watu wanakosea.

“Japokuwa, hili halijawahi kuharibu kiwango chetu. Wachezaji wato ni wazuri na wanahitaji ushindi. Lakini, kama kocha ataanza kuharibu hili ndio kinatokea alichokizungumza raisi.

“Hakuna mtu aliyewahi kuwa na mashaka na uwezo wake kama kocha, lakini kulikuwa na hili tatizo. Mwisho wa siku, tulileta kombe nyumbani, kitu ambacho huwezi kukichukulia poa.”

Juve walibeba kombe kwa tofauti ya pointi 1 dhidi ya Inter Millan japokuwa mashabiki wa timu hiyo hawakupendezwa na namna ya uchezaji wa timu hiyo.


Ondoka na Mkwanja Kwenye Tsh. 160,000,000

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu.

Soma Zaidi

24 Komentara

    Sarr kocha mzuri sema hana bahat

    Jibu

    Ni kocha mzuri tu.

    Jibu

    Sarri hanaga jipya kwny soka vilabu vyote alivyopita vyote katimulawah tu

    Jibu

    Imeeleweka

    Jibu

    Ttz hana nyota

    Jibu

    Hana maajabu huyo

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Ishakuwa shida kwake sasa

    Jibu

    Kwa nn? sasa anakosa kuwaamin

    Jibu

    Asante kwa taarifa meridian

    Jibu

    Sarr ni kocha mzuri ila hakua na maelewano mazuri na wachezaji wake

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Namkubali Sana huyo kocha anajua nini anakifanya

    Jibu

    Kocha mwenye maamuzi yake ayumbichwi

    Jibu

    Sarri hana jipya

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Kocha yupo vizuri

    Jibu

    Sarri ni kocha makini sana

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Kocha yuko vzr sana

    Jibu

    Ila hawakufanya poa kwa kweli

    Jibu

    Daaah!!

    Jibu

    Namkubali Sana huyo kocha anajua nini anakifanya

    Jibu

    Sarr ni kocha mzuri sema kwa msimu wa mwaka jana Juve walimuangusha kocha wao

    Jibu

Acha ujumbe